Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki Dar wagoma

Muktasari:

Wafanyakazi hao wamechukua uamuzi huo baada ya kushinda kesi ya madai waliyofungua mwaka 2008 dhidi ya mwajiri wao aliyekuwa ameshindwa kutekeleza malipo ya mshahara katika viwango vipya vilivyotangazwa na serikali mwaka 2007.

Dar es Salaam. Zaidi ya Wafanyakazi 1, 200 wa kiwanda cha Tanzania China-Friendships Co. Ltd (Urafiki) wameanza mgomo leo kushinikiza nyongeza ya mshahara na mazingira bora ya kazi.
Wafanyakazi hao wamechukua uamuzi huo baada ya kushinda kesi ya madai waliyofungua mwaka 2008 dhidi ya mwajiri wao aliyekuwa ameshindwa kutekeleza malipo ya mshahara katika viwango vipya vilivyotangazwa na serikali mwaka 2007.
Wakizungumza kiwandani hapo, wafanyakazi hao ambao walisikika wakiimba nyimbo za kumtaka Rais John Magufuli afike kiwandani hapo kusaidia kutatua mgogoro huo walisema kwa mujibu wa sheria na taratibu wanapaswa kulipwa shilingi 210, 000 badala ya Sh100,000 wanayolipwa sasa.
Wamesema kima cha chini cha mshahara kinapaswa kupanda kutoka Sh100,000  hadi Sh150,000 kwa mwezi huku wakitakiwa kulipwa posho ya Sh60,000 kwa mwezi.
Kutokana na madai hayo kupuuzwa, wafanyakazi hao wameahidi kuendelea na mgomo huo hadi uongozi utakapowaeleza hatma ya madai yao.
Akizungumza kiwandani hapo, Naibu Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Moses Swai amesema uongozi umeshangazwa na hatua ya wafanyakazi kugoma wakati suala la madai ya mishahara yao lipo kwenye Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA).
Amesema uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kazi Febuari mwaka huu ulikitaka kiwanda hicho kulipa malimbikizo na viwango vipya vya mshahara kwa wafanyakazi hao, lakini wakashindwa kuafikiana kuhusu kiwango halisi cha fedha ambacho walipaswa kulipa.
“Sisi kama menejimenti tulipiga mahesabu na kuona tunatakiwa kulipa