Wagonjwa 40,000 wagundulika kuwa na sonona nchini
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Muktasari:
Hata hivyo hii ni idadi ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa tatizo linavyokisiwa.
Dar es Salaam. Taarifa ya hali ya afya ya magonjwa ya akili ya mwaka 2015/16 nchini Tanzania inaonyesha kuwa takribani wagonjwa 41,789 waligundulika kuwa na tatizo la sonona.
Hata hivyo hii ni idadi ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa tatizo linavyokisiwa.
Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu imesema sababu ya kutokuwa na takwimu za kutosha ni wagonjwa wachache wanao hudhuria katika vituo vya kutolea huduma kwa matatizo mbalimbali ya afya ya akili na matatizo ya kisaikolojia hapa nchini.
"Ziko sababu mbalimbali ambazo hupelekea jamii kupata ugonjwa wa sonona. Sababu hizi zimegawanywa katika makundi makubwa matatu, ikiwemo kibailojia, kisaikolojia na kijamii," amesema.