Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahamiaji haramu 62 kutoka Ethiopia wadakwa Mufindi

Wahamiaji 62 raia wa Ethiopia waliokamatwa akiwa kwenye gari hilo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya. Picha na Mary Sanyiwa

Muktasari:

  • Wahamiaji hao walikuwa wamepanda lori aina ya Scania lenye namba za usajili T631 CNF lililokuwa na treila lenye namba T531 DGE.

Mufindi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 62, raia wa Ethiopia, kwa kosa la kuingia nchini bila kibali pamoja na dereva wao, Boniface Mwanjokolo (42), mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam aliyekuwa akiwasafirisha.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Agosti 22, 2024 mjini Mufindi mkoani Iringa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea Agosti 21, 2024 saa 3 usiku katika eneo la Sabasaba, Mafinga wilayani Mufindi.

Kamanda Bukumbi amesema wahamiaji hao walikuwa wamepanda lori aina ya Scania lenye namba za usajili T631 CNF lililokuwa na treila lenye namba T531 DGE.

Amesema gari hilo lilikuwa limebeba mabomba ya kupitishia maji machafu kutoka Dar es Salaam kwenda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Amesema baada ya kufanya upekuzi kwenye gari hilo, walibaini kuwa katikati ya mzigo huo wa mabomba, kulikuwa na  sehemu yenye uwazi ambapo wahamiaji hao walikuwa wamefichwa wakisafirishwa kuelekea Kyela.

“Baada ya kufanya upekuzi, tulifanikiwa kubaini katikati ya mzigo huo kuna sehemu chini ya gari hilo kuna uwazi ambao raia hao 62 kutoka Ethiopia walikuwa wamefichwa wakisafirishwa kuelea Kyela mkoani Mbeya,” amesema Bukumbi.

Kamanda huyo amefafanua kuwa baada ya kuwakamata wamekabidhiwa  kwa Jeshi la Uhamiaji kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kushirikiana na Ofisi ya Mashtaka.