Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahitimu mafunzo ya misitu waaswa kujiajiri

Muktasari:

  • Wahitimu wa mafunzo stadi ya misitu na uchakataji wa mbao wameshauriwa kujiunga vikundi na kuoata mikopo kufungua viwanda vyao.

Mafinga. Wahitimu wa mafunzo stadi ya wahudumu wa misitu na uchakataji wa mazao ya mbao, wameshauriwa kujiunga katika vikundi na kuomba mkopo katika halmashauri na kufungua viwanda vyao na sio kusubiri kuajiriwa.

Ushauri huo umetolewa leo Januari 24 na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji Ufugaji Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Daniel Pancras wakati wa mahafali ya mafunzo stadi ya wahudumu wa misitu na uchakataji mazao ya mbao yalifanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Viwanda vya Misitu- Mafinga (FWITC).

Pancras amewataka wahitimu hao kuanzisha vikundi vya ujasiliamali na kuwa wabunifu zaidi na wasitegemee kuanjiriwa kwani wanafunzi wanaomaliza katika vyuo mbalimbali nchini ni wengi na ajiri katika sekta rasmi ni chache.

Pancras amesema kuwa lengo kuu la serikali la kuanzisha vyuo vya maafunzo ya ufundi stadi (VETA) ni kuwasaidia wananchi ambao hawakufanyikiwa kuendelea na elimu ya ngazi ya vyuo vikuu waweze kapata ujuzi, ambao wakiwezeshwa kwa kupewa taaluma ya vitendo wanaweza kujiajiri wenyewe.

“Mimi hapa naiona ajira kwenu yaani nyinyi kuwaajiri watu wengine kwa kuwa Wilaya ya Mufindi kuna fursa nyingi vya viwanda vya misitu na mnaweza kutumika kama wataalamu,” ameelezea.

Naye mmoja wa wanzilishi wa mradi wa Pandamiti Kibiasahra na pamoja na kituo cha mafunzo ya viwanda vya misitu- Mafinga (FWITC), Ben Sulusi amewapongeza wahitimu hao kwa mwitikio wa kujiunga na mafunzo.

Amesema kuwa wahitimu hao watasaidia kupeleka sekta ya misiti mbele na kupongeza serikali ya Finland kupitia wizara ya mamabo ya nje kwa ushirikianan wa miaka kumi iliyopita na kwa kuwezesha kupeleka rasilimali.

Kwa upande wao, wahitimu wamezipongeza Serikali za Tanzania na Finland kupitia mradi wa Pandamiti Kibiashara (PFP) kwa kuwezesha kuwepo kwa kozi hiyo ya mafunzo stadi ya wahudumu wa misitu na uchakataji wa mazao ya mbao katika ngazi chini.

Kwa upande wake Zawadi Nelson ambaye ni mhitimu katika Chuo cha Misitu – Arusha, wamewashukuru wadau wa mradi wa Pandamiti Kibiashara kwa kushirikiana na serikali kwa ufadhili huo wa mafunzo na kuiomba serikali iwatazame katika jicho la huruma kwa sababu wataalamu wa masuala ya misitu kwa upande wa wanawake ni wachache.