Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakazi Kata ya Myunga wajivunia kupata Chuo cha DIT

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa uwepo wa Chuo cha Ufundi DIT katika Kampasi ya Myunga Kata ya Myunga, Wilaya ya Momba mkoani Songwe umeleta neema na mwamko wa mabadiliko ya maendeleo katika kata.

Songwe. Imeelezwa kuwa uwepo wa Chuo cha Ufundi DIT katika Kampasi ya Myunga Kata ya Myunga, Wilaya ya Momba mkoani Songwe umeleta neema na mwamko wa mabadiliko ya maendeleo katika kata.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Februari 22, 2022 wamesema uwepo wa chuo hicho umekuwa na mabadiliko makubwa yakiwemo kuongezeka kwa watu ambao wamechangia kupanuka kwa biashara katika eneo hilo.

Amos Philmoni mkazi wa kata hiyo amesema chuo hicho kimetoa fura kwa vijana kujifunza stadi za ufundi wanaotumia kujiajiri wenyewe.

"Tumepata elimu yenye ujuzi na tunajiamini tunaweza kufanya kazi sehemu yoyote na hatuchagui kazi jamii imetupokea na inatupa ushirikiano kwa kutupatia ajira ndogondogo"amesema Amosi.

Mariam Andrew mjasiriamali anayeuza chakula (mama lishe) amesema siku za hivi karibuni tangu kuanza kwa chuo hicho biashara yake imepata wateja wakiwemo wageni na wanafunzi.

Naye Mkuu wa wa Taasisi ya DIT Kampasi ya Myunga, Preksedis Ndomba amesema ujuzi unaotolewa kwa wanafunzi chuoni hapo ni wa uhakika na wanachuo wanaweza kufanya kazi sehemu yoyote kwa ufanisi zaidi.

Katika mahafali ya mwaka huu, jumla ya wanafunzi 65 wamehitimu mafunzo  kwa ngazi ya ujenzi na mafunzo ya ufundi stadi ambayo yatawasaidia wahitimu kujiajili.