Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima kutumia bundi kudhibiti panya shambani

Muktasari:

Wakulima zaidi ya 200 kutoka katika wilaya ya Iringa na Mufindi Mkoani Iringa wamepewa mafunzo kuhusu matumizi ya bundi kudhibiti visumbufu vya mazao mashambani na kuacha kumuhusisha bundi na imani za kishirikina.

Iringa. Wakulima zaidi ya 200 kutoka katika wilaya ya Iringa na Mufindi Mkoani Iringa wamepewa mafunzo kuhusu matumizi ya bundi kudhibiti visumbufu vya mazao mashambani na kuacha kumuhusisha bundi na imani za kishirikina.

Akitoa mafunzo hayo leo Jumatatu Mei 30, 2022 katika Kijiji cha Mgama wilaya ya Iring, Dk Nikolaus Mwalusaka kutoka chuo cha SUA ambaye ni Mtafiti Mkuu wa mradi unaohusu uelewa mtazamo wa wakulima kuhusu kutumia bundi kukabiliana na viumbe wasumbufu wa mazao hasa panya.

Dk Mwalukasa amesema lengo kuu la utafiti huo ni baada ya kuwa na upotevu wa mahindi kwa asilimia 5-15 kwa mwaka kutokana na panya wanaokula mahindi, sababu mazingira yanawezesha panya kuzaliana na kukua kwa kasi kubwa.

Amesema wakulima wamekuwa wakitumia dawa za kemikali kuthibiti panya mashambani huku utumiaji wa kemikali si rafiki kwa mazingira na kuwa na madara kwa binadamu.

Amesema moja ya mikakati inayotiliwa mkazo na Serikali pamoja na watafiti ni kutumia njia mbadala kudhibiti viumbe waharibifu ambayo ni rafiki kwa mazingira.

“Tumefanya utafiti wa kuja na mbinu mbadala ambayo ni rafiki na mazingira lakini inasaidia kukabiliana na panya ambao ni kutumia bundi, Utafiti wetu umekuja kuelimisha wakulima ni namna gani wanaweza kutumia bundi katika kukabiliana na visumbufu vya mazao ambao ni panya”

Amesema wamewafundisha wakulima namna ya kufanya ili kuwezesha bundi kukabiliana na viumbe visumbufu ni kuwatengenezea viota ambavyo vitawekwa kwenye mashamba.

“Sababu ya kuweka viota mashambani ni kwa kuwa bundi ni ndege ambaye hapendi kutengeneza viota vyake ili yeye aweze kupatikana kwenye mashamba tunamtengenezea kiota na bundi atahamia kwenye kile kiota na kufanya makazi yake”.

“Wakati wa mchana atakuwa anakaa kwenye kiota na wakati wa usiku atakuwa anatoka kwenda kutafuta chakula chake, na chakula ambacho bundi anapenda sana ni panya, kwa hiyo bundi atatoka kwenda kutafuta panya na wakati huo atakuwa anapunguza panya ambao ni visumbufu vya mazao kwa wakulima”

Akizungumza mmoja wa wakulima kutoka katika Kijiji cha Mgama wilayani Iringa, Aidani Kisinga amesema wamefurahishwa na elimu hiyo na kwamba bundi ni mnyama ambaye ni rafiki anayeweza kusaidia kula panya ambavyo ni visumbufu vya mazao.

“Wakulima wengi tumekuwa na muitikio mzuri na tunashukuru kupata elimu hii kwa sababu wengi tulikuwa na Imani kwamba bundi anahusiana na mambo ya uchawi”amesema.

Amesema baada ya kupewa elimu kuwa bundi anakula panya ambao ni visumbufu vya mazao wengi wamekuwa na muitikio mzuri na wamekubali kuieneza hii elimu kwa wengine zaidi ili kuweza kuwaondoa katika hiyo fikra potofu ambayo wanayo.

Kwa upande wake Anna Kimaro Mtafiti kutoka SUA kwenye mradi unaohusu jinsi gani wanaweza kutumia bundi kukabiliana na viharibifu vya mazao hususani zao la mahindi amewataka wananchi kuacha fikra potofu kuwa bundi anatumika katika masuala ya kishirikina.

“Tumefanya utafiti tumegundua bundi hatumiki katika masuala ya kishirikina lakini bundi jinsi alivyo anatumia milio na sauti mbalimbali kuwasiliana na bundi wenzake” amesema