Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliochepusha marobota ya vitenge wapandishwa kizimbani

Watu saba wafikishwa kortini wakidaiwa kujipatia Sh 428milioni mali ya Tanesco

Muktasari:

  • Watu watatu akiwemo mkurugenzi wa Kampuni ya Dewa Trading, Erasto Dewa (54) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na manne likiwemo la kukwepa Kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh487.9 milioni.

Dar es Salaam. Watu watatu akiwemo mkurugenzi wa Kampuni ya Dewa Trading, Erasto Dewa (54) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini hapa wakikabiliwa na manne likiwemo la kukwepa kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh487.9 milioni.

Mali na Dewa wengine ni mfanyabiashara, Ramadhan Salum (24) ambaye Mkazi wa Tabata Segerea na mfanyabiashara Frank Mgata (35) ni Mkazi wa Keko Mwanga.

Hivi karibuni TRA ilitoa taarifa ya kukamata marobota ya vitenge yaliyokuwa yakisafirishwa nje, lakini yakachepushwa kuelekea Tabana na mengine Kariakoo.

Akiwasilisha mashitaka leo Novemba 10, Wakili Mwandamizi wa TRA, Medalaki Emanuel amedai mbele ya Hakimu Mwandamizi, Francis Mhina kuwa washtakiwa hao wanakabiwa na shitaka la uhujumu uchumi yenye mashtaka manne la kukwepa Kodi, kuchepusha bidhaa kutoka kwenye njia yake, kutumia njia ya uongo na kuisababishia hasara TRA.

Ameendelea kudai kuwa Septemba 21, 2022 maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja walihusika na udanganyifu kwa kutoa taarifa za uongo kuwa shehena ya marobota ya shuka 290 ilikuwa inasafirishwa kwenda nchini Malawi Lilongwe lakini waliitelekeza shehena hiyo Tabata yenye thamani ya zaidi ya Sh487.94 milioni.

Katika shtaka la tatu Septemba 28, 2022  maeneo hayo, wote kwa pamoja walifanya ulaghai Kwa kuchepusha bidhaa za vitenge kutoka Dar es Salaam kwenda Malawi na kupakia bidhaa hizo katika eneo la Tabata jijini humo.

Emanuel alidai shtaka lingine inadaiwa Septemba 21, 2022 maeneo ya bandari ya Dar es Salaam mshtakiwa Dewa kwa udanganyifu akitoa tamko la uongo la maelezo ya shehena ya marobota 290 kama mashuka badala ya vitenge.

Katika shtaka la mwisho inadaiwa Septemba 28, 2022 maeneo ya Tabata wote kwa pamoja walikwepa kodi na kuisababishia TRA hasara ya zaidi ya Sh487.9 milioni.

Alidai upelelezi wa shauri Hilo bado haujakamilika na aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine Kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina alisema kutokana na mashtaka wanayokabiliwa nayo nibya uhujumu uchumi hayana dhamana hivyo hawatajiwi kujibu chochote.

Mhina aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 24, 2022 Kwa ajili ya kutajwa huku washtakiwa hao wakipelekwa mahabusu.