Waliochukua fomu za uspika CCM wafikia 66

Muktasari:

  • Ikiwa imebaki siku moja kabla ya kufungwa kwa dirisha la wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanachama 66 wa CCM wameshajitokeza na kuchukua fomu katika vituo vya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

Dodoma. Iki Ikiwa imebaki siku moja kabla ya kufungwa kwa dirisha la wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanachama 66 wa CCM wameshajitokeza na kuchukua fomu katika vituo vya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika Job Ndugai Januari 6, baada ya kutoa kauli zilizopishana na Rais Samia Suluhu Hassan na baadaye kushinikizwa na makada wa chama hicho kujiuzulu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 14, Katibu Msaidizi mkuu wa Oganaizesheni ya CCM, Solomon Itunda amesema kwa leo tu wamejitokeza wana CCM 17 kuchukua fomu huku ambapo watatu wamechukulia Ofisi kuu Dodoma, 12 Dar es Salaam na wawili ofisi ya Zanzibar.

"Wanachama waliochukuia fomu leo Januari 14, 2022 Kwa Dodoma ni Hatibu Madata Mgeja, Dk Linda Ole Saitabau na Profesa Norman Sigalla King," amesema Itunda.

Amewataja wengine waliochukulia Ofisi Ndogo ya Dar es Salaam ni Emmanuel Sendama, Dk Thomas Kashilila, Goodluck Mlinga, Bibie Msumi, Hilal Seif na Athumani Mfutakamba.

Wengine ni Mwenda Mwenda,  Herry Kessy, Josephat Malima, Adamu Mnyavanu, Stella Manyanya na Andrew Kevela.

Kwa upande wa Zanzibar wamechukua wanachama wawili ambao ni Luhaga Mpina na Hussein  Mataka hivyo kufanya jumla ya waliochukua fomu hadi leo kuwa 66.