Wanafunzi 400 wanakaa chini, wanatumia chumba kimoja cha darasa

Wanafunzi 400 wanakaa chini, wanatumia chumba kimoja cha darasa

Muktasari:

  • Wanafunzi zaidi ya 400 wa darasa la nne na tano wanakaa  chini na kutumia  chumba kimoja cha darasa kwenye Shule ya Msingi Bugumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Sengerema.Wanafunzi zaidi ya 400 wa darasa la nne na tano wanakaa  chini na kutumia  chumba kimoja cha darasa kwenye Shule ya Msingi Bugumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo,  Paul Vicent amesema shule hiyo ina walimu 30 na wanafunzi  3, 118 kuanzia darasa la awali hadi la saba.

Amesema sababu ya kukaa chini ni idadi kubwa ya wanafunzi  licha ya Serikali kutoka Sh71 milioni kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Mbunge wa  Sengerema,   Hamisi Tabasamu amesikitishwa na hali hiyo licha ya  kutoka ushauri kuwa fedha  hizo zitumike kujenga shule nyingine ili kuondoa msongamano huo.

Tabasamu amesema  ushauri wake ulipuuzwa na viongozi wa Halmashauri hiyo huku akimnyooshea kidogo ofisa elimu msingi Halmashauri ya Sengerema,   Donalt Bunonosi kuwa ndiye aliyesababisha hali hiyo kwa kupuuza ushauri.

Wanafunzi 400 wanakaa chini, wanatumia chumba kimoja cha darasa

Naye Bunonosi amesema hakuwa na  maelekezo ya fedha kutumika  kujenga shule nyingine bali alikuwa na maelekezo ya kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chifunfu,   Dominic Tilosahu amesema wataalamu hawana ushirikiano na wananchi na ndio sababu ya shule hiyo kuendelea kuwa na wanafunzi wanaokaa  chini.

Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema,   Ally Salim amesema watazifanyia kazi changamoto za shule hiyo na kuzipatia ufumbuzi.