Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi wanne wajeruhiwa ajalini, 16 wakinusurika

New Content Item (1)

Gari lililokuwa limebeba wanafunzi wa shule ya msingi, FM Foundation likiwa limetumbukia korongoni, eneo la Bonite, Manispaa ya Moshi.

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea leo  Februari 11, 2026 baada ya gari aina ya Toyota haice walilokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kutumbukia korongoni, eneo la Bonite, kata ya Shirimatunda, Manispaa ya Moshi.

Moshi. Wanafunzi 16 wa Shule ya Msingi FM Foundation iliyopo Manispaa ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro wamenusurika baada ya gari aina ya Toyota Hiace walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuangukia korongoni bada ya  kukosa mwelekeo.

Katika ajali hiyo, watu wanne wamejeruhiwa wakiwamo wanafunzi wawili wa shule hiyo, dereva wa gari na msaidizi wake.

Majeruhi hao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Gadaffi Masoud amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza imetokea leo Jumatano asubuhi, Februari 11, 2026 katika eneo la Bonite, Kata ya Shirima Matunda, Manispaa ya Moshi.

Amesema jeshi hilo lilipokea taarifa za gari hilo lililokuwa limewabeba wanafunzi kuanguka korongoni katika Mtaa wa Bonite na kikosi cha uokoaji kilifika haraka katika eneo la tukio.

“Baada ya kupokea taarifa, tulifika eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji na tulikuta wananchi tayari wakisaidia kuwaondoa watoto ndani ya gari hilo. Tuliwachukua majeruhi na kuwapeleka Hospitali ya Mawenzi kwa matibabu zaidi,” amesema Masoud.

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Masoud amesema uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na hitilafu katika mfumo wa usukani hali iliyosababisha kujifunga wakati gari likiwa kwenye mwendo.

Amesema hitilafu hiyo ilisababisha dereva kupoteza udhibiti wa gari, hatimaye kuacha njia na kuanguka korongoni.

“Mpaka sasa watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wanaendelea kupatiwa matibabu. Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo kamili cha tukio hilo,” amesema Masoud.