Wananchi waonywa kuvua na kuuza nyama ya nyangumi
Moja kati ya mnyama Nyangumi wakicheza baharini kstika eneo la Mnazibay Mtwara. Picha na Florence Sanawa
Muktasari:
- Baada ya wananchi wa Kijiji cha Mkungu kugawana nyama ya nyangumi kwa siku mbili, Marine Park waonya wavuvi wanaovua mnyama huyo kwa kuwa ni kinyume cha sheria ambapo inaweza kusababisha faini/kifungo ama vyote kwa pamoja kwa atakayekutwa nae.
Mtwara. Siku chache baada ya mkoa wa Mtwara kuzindua utalii wa mnyama nyangumi ambapo uzinduzi huo ulifanyika Agosti 5 mwaka huu, siku ya juzi wananchi wa Kijiji cha Mkungu, Kata ya Naumbu wamegawana nyama ya mnayama huyo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha mkungu kata ya naumbu halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wakimalizia kugawana nyama ya mnyama nyagumi. Picha na Florence Sanawa
Akizungumza na Mwananchi, Mhifadhi wa bahari ghuba ya Mnazi na maingilio ya Mto Ruvuma (Marine Park), Paulo Nyige amesema kuwa sheria ipo ya nchi na ya kimataifa ambapo zinaitaka nchi kuwalinda viumbe ambao wako katika hatari ya kutoweka akiwemo nyangumi.
Amesema kuwa sheria zipo wazi ya hifadhi namba 29/1994 na imeweka wazi na imezuia kufanya shughuli zozote za uvuvi kwa viumbe bahari ambavyo vipo hatarini kutoweka akiwemo nyangumi sheria imekataza wazi nyangumi ni nyara ya Serikali.
“Wananchi wanapaswa wafahamu kuwa nyngumi analindwa endapo mtu akikutwa na mnyama nyangumi cha kwanza anashtakiwa na zipo faini ama kifungo ama vyote kwa pamoja hata Sheria 2003 imezuia kujihusisha na bishara hiyo ambapo nchi pia imeiangia mikataba ya kimataifa ya kuwalinda hawa viumbe ni makubaliana ambayo tumeingia kuwalinda viumbe hawa” amesema Nyige.
Naye Omary Mtiko ambaye ni mvuvi wa Naumbu amesema kuwa samaki huyo alichukua nyavu zao wakati wanavua ndio kutokana na kuchukua nyavu hizo walifanikiwa kumvua na kutoa habarini.
“Wakati huu ndio msimu wa mnyama nyangumi ambapo ambapo huanzia mwishoni mwa mwezi Julai na huwa kwa makundi na huenda mpaka mwezi mwezi Novemba huenda sambamba na msimu wa embe mbichi (ndolo) ndio wanawanakuwa wanakuja juu ni mara yetu ya kwanza sisi kumpata hautajawahi kumpata,” alisema Mtiko.
Tatu Madizi mkazi wa Naumbu, alisema kuwa samaki kwa maelelezo ya wavuvi mnyama huyo alinasa kwenye vyombo vinne na wakashindwa kumbeba hivyo kulazimika kumchinjia huko huko.
Aidha Haji Yusuph mvuvi alikana kuvua mnyama huyo na kusema kuwa yeye alikutana na wanawake ambao walikuwa wanatoka baharini na kusema kuwa wao ndio walimpa taarifa ya uwepo wa samaki huyo kando ya bahari.
“Huyu nyangumi hajavuliwa kama kuvuliwa alisukumwa na maji kutoka baharini akaletwa kando ya bahari kwa kweli amejichanganya mwenyewe akajipiga kwenye mwamba akarushwa pwani na akiwa pwani kuna wanawake walimuona wakaja kutoa taarifa kuwa wamemuona mdudu wakasema hawamjui,” amesema.
Salum Issa mvuvi amesema kuwa mnyama huyo alionwa na wanawake ndiyo walitupa taarifa na sisi tulifika ndio wao msimu wao wapo wengi hatujamvua.