Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaodaiwa kutumia Nida za wenzao kusajilia laini, waendelea kusota rumande

Washtakiwa wanaodaiwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine kujipatia fedha, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Nyamitah na wenzake watano, wanadaiwa kutenda makosa kati ya Mei mosi, 2025 na Aprili 2026 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dar es Salaam. Upelelezi kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara na mkazi wa Madale, Gilbert Nyamitah (33) na wenzake watano, haujakamilika.

Nyamitah na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 yakiwamo ya kuongoza genge la uhalifu na kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine kujipatia fedha.

Pia, wanadaiwa kutumia vitambulisho vya Taifa (Nida) vya watu mbalimbali kusajilia laini za simu za watu tofauti kinyume cha sheria na kutakatisha Sh355 milioni.

Wakili wa Serikali, Titus Aron ametoa taarifa hiyo leo Jumatatu, Mei 18, 2026 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Washtakiwa wanaodaiwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine kujipatia fedha, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha Hadija Jumanne

Mbali na Nyamitah, washtakiwa wengine ni Fabian Kulwa (40) Mbezi Makabe, Mnyamisi Selumamala (34) mkazi wa Musoma mkoani Mara, Salum Kapene (31) mkazi wa Nyamanoro mkoani Mwanza, Onesmo Aron (34) Mkazi wa Runzewe mkoani Geita na Joram Fanuel (23) mkazi wa Tarime mkoani Mara.

"Kesi hii imeitwa kwa kutajwa na upelelezi wake bado unaendelea, kwa sababu hiyo, tunaomba Mahakama itupangie tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai wakili Aron.

Hata hivyo, hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, alikubaliana na ombi la Jamhuri na kuahirisha hadi Juni Mosi, 2026 kwa ajili ya kutajwa.

Kesi hiyo imesikilizwa kwa njia ya video, huku washtakiwa wakiwa rumande.

Pia, shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili, halina dhamana hivyo wataendelea kusalia rumande hadi upelelezi utakapokamilika.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Mei 4, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 9426 ya mwaka 2026.

Katika mashtaka 28 yanayowakabili; 16 ni ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine; mashtaka 10 ni ya kutumia Nida ya mtu mwingine kusajilia laini za simu; moja ni kuongoza genge na jingine ni kutakatisha fedha kiasi cha Sh355 milioni.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika shtaka la kuongoza genge la uhalifu linalowakabili wote, wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Mei mosi 2025 na Aprili 2026, eneo lisilojulikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa wanaodaiwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine kujipatia fedha, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha Hadija Jumanne

Shtaka la pili hadi la 17, ni kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine, mashtaka yanayomkabili Nyamitah peke yake.

Nyamitah, anadaiwa kutenda makosa hayo Machi 31, 2026 eneo la Madale, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa huyo alitumia laini 16 za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu tofauti bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wakati akijua ni kinyume cha sheria.

Baadhi ya laini za simu alizotumia zilikuwa zimesajilia kwa jina la Daniel Matiko, Chacha Marwa, Zainabu Burunya, Manga Manga, Boke Mwita na wengine.

Shtaka la 18 hadi la 27 ni kutumia vibaya taarifa za wateja kwa kutumia kitambulisho cha Nida kusajilia laini za simu bila ridhaa yao na kinyume cha sheria, shtaka linalomkabili mshtakiwa Fanuel pekee yake.

Fanuel, anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 28, 2025 hadi Agosti 21, 2025 katika maeneo ya Nyanjage- Gachuma (Tarime), Busega na Rorya, akiwa wakala wa Kampuni ya Honora Tanzania PCL aliyesajiliwa kwa jina la Roza Stivin Magoiga, alitumia vibaya vitambulisho 10 vya Nida vya watu wengine kusajilia laini mbalimbali za simu, kinyume cha sheria.

Shtaka la 28 ni kutakatisha fedha linalomkabili mshtakiwa Nyamitah na Kulwa, wanaodaiwa kulitenda katika tarehe tofauti kati ya Mei mosi, 2025 na Aprili 2026 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walijipatia Sh355 milioni kwa usajili wa laini, wakati wakijua makosa hayo ni ya zao tangulizi la kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine.