Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaume watakiwa kuwashirikisha wake zao umiliki wa ardhi

Muktasari:

Imeelezwa kuwa migogoro mingi ya ardhi na mirathi inawaathiri wanawake kwa sababu ya kutoshirikishwa na waume zao katika umiliki wa radhi.

Iringa. Wanaume mkoani Iringa wameshauriwa kuwashirikisha wenza wao katika umiliki wa ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi na kupunguza kesi za mirathi mkoani hapo pindi wanapofariki.

Rai hiyo imetolewa leo Julai 20 na Mkurugenzi wa shirika la Landesa Tanzania, Godfrey Massay wakati wa mafunzo kwa wapima ardhi wasaidizi 20 kutoka katika Kijiji cha Ikongosi na Ikongosi juu wilayani Mufindi ambapo shirika hilo linatarajia kutoa hati za kimila zaidi ya 2000.

Massay amesema migogoro mingi ya ardhi inatokea kwa vyanzo vyingi hasa masuala ya mirathi na kusababisha wanawake kunyanyasika kwa sababu wanaume au wenza wao hawana utamaduni wa kuwashirikisha katika umiliki wa ardhi.

“Mfumo dume ambao tunao umefanya kwamba ardhi inamilikiwa na mwanaume tu na mwanamke anaweza kumiliki ardhi kupitia mwanaume, changamoto ni pale ambapo mweza anapofariki mwanamke yule kama hakukuwa na utaratibu mzuri uliowekwa basi mwanamke huyo anaachwa katika wakati mgumu.

“Ardhi hiyo ni rahisi sana kuchukuliwa na ndugu wa kiume kwa niaba ya familia iyo na mwanamke akibaki ananyanyasika watu wengi hawana utamaduni wa kuandika wosia hivyo wanapokuwa wamefariki mali hizo hugombaniwa na waliobaki ikiwemo wenzi wao, watoto na ndugu wa karibu,” amesema Massay.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi Mkuu wa dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa, Elizabeth Swai amesema kuna mila na desturi zimemnyima haki ya kumiliki ardhi mwanamke kutokana na elimu kutofika hasa vijijini.

“Elimu itolewe kwa wanandoa na wanafamilia wote hasa vijijini kuwa ni haki ya kila mtu kumiliki ardhi iwe ni kwa kugawana, kwa pamoja au kwa hisa ili moja anapotangulia kufa mwingine apate haki yake na kuepuka migogoro ndani ya wanafamilia,” amesema.

Naye wakili wa Mahakama kuu na mtaalam wa masuala ya ardhi kutoka shirika la Landesa ofisi ya Tanzania, Masalu Luhula amesema kuwa umiliki wa ardhi kwa sasa unazingatia masuala ya usawa wa kijinsia katika kujilinda na ukatili na unyanyasaji katika ngazi ya jamii hasa pale mweza mmoja anapotangulia kufariki bila kuacha wosia katika familia yake.

“Kunapokuwa na ushiriki wa pamoja katika umiliki wa ardhi kwenye ndoa inasaidia kuondoa migogoro mingi ya ardhi inayotokana na familia kugombania mali za marehemu na kuiacha familia ya marehemu ikiteseka.”

Akifafanua kauli hiyo, Ofisa program masuala ya haki za ardhi katika shirika la Pelum Tanzania, Angolile Rayson amesema toka mfumo wa sheria ya ardhi 1999 mwanamke na wanaume wanayohaki sawa kutumia kupata na kufanyia shughuli yeyote katika masuala ya ardhi bila kikwazo cha aina yeyote.

“Mipango mingi ya ulasimishaji wa ardhi vijijini tunaanza na elimu na kufanya mipango ya matumizi ya ardhi na kutoa hati ambapo tumeweka vipaumbele kuwa ni pamoja na wakina mama wajane na wale ambao wanakipato duni hii yote ni kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi ya kumiliki ardhi,” amesema.