Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake watakiwa kujiamini, kuacha kulaumu historia

Rasi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Profesa Esther Dungumaro (katikati) akizungumza na wanawake katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika chuo hicho.

Muktasari:

Rasi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu cha Mkwawa, Profesa Esther Dungumaro amewataka wanawake kupaza sauti na kujiamini katika mawazo yao katika jamii.

Iringa. Rasi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu cha Mkwawa, Profesa Esther Dungumaro amewataka wanawake kupaza sauti na kujiamini katika mawazo yao katika jamii.

Pia, wametakiwa kuacha kulaumu historia na kuendelea kushikilia mila na desturi potofu za kuamini kuwa wanaonewa na kudhalilishwa.

Dungumaro amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa.

"Historia iachwe kuwa historia isitumike sasa ndio tumeshikia bango kwamba wanamke wanaonewa hakuna kitu kama hicho, tunaishi katika Tanzania yetu huru yenye fursa sawa kwa wote"

"Tuendelee kujiamini na kujituma kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika na kuonyesha weledi katika kazi ambazo tunafanya kwani mafanikio yatakuja, wanawake waanze kujiamini na kupaza sauti zao na kuacha kulaumu historia" amesema

Mshiriki mwalikwa katika maadhimisho hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Eugenia Kafanabo Mgeni amesema ni wakati wa mwanamke tutekeleza majukumu yake kwa faida ya maendeleo yake mwenyewe.

"Tusiogope kufanya kazi kwa bidii na kwa kisingizio cha sisi ni wanawake sasa hivi dunia imebadilika juhudi na weledi kazini ndio chanzo cha mafaanikio yako" amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Polisi Jinsia, Wanawake na Watoto Mkoa wa Iringa, Elizabeth Swai amewataka wanawake kufichua ukatili na unyanyasaji wanaofanyiwa ili wapewe haki zao na kumaliza tatizo la ukatili kwa wanawake na watoto.

"Kuna baadhi ya wanawake wanafanyiwa ukatili huko kwenye ndoa zao wanakaa kimya kwa kuvumilia wakiamini mwanaume atabadilika kumbe ndio unalikuza tatizo na kulifanya kuwa kubwa kiasi cha siku ikifika mwisho unasikia amepigwa kibao ameanguka akafariki hivyo tufichue ukatili huu ili ukomeshwe" amesema