Wanne mbaroni kwa kupatikana na magamba ya kakakuona

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika Mtaa wa Reli, Kata ya Kichangani mjini hapa kwenye ghala la mashine ya kukobolea nafaka

Morogoro. Polisi mkoani hapa inawashikilia watu wanne, wakiwamo raia wa Burundi watatu wakituhumiwa kupatikana na magamba 1,000 ya kakakuona ambayo ni sawa na wanyama hao 670.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika Mtaa wa Reli, Kata ya Kichangani mjini hapa kwenye ghala la mashine ya kukobolea nafaka.

“Magamba ya mnyama huyo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye mifuko ya kilo 50 na kutumbukizwa kwenye viroba vya kilo 100 vilivyochanganywa na maharage,” alisema kamanda Matei.