Wanyanga Chemba wachangia damu

Baadhi ya mashabiki wa timu ya yanga Kijiji cha Olboloti wilayani Chemba wakichangia damu salama ili kuokoa maisha ya mama na mtoto kufuatia timu yao kufanya vizuri, jumla ya uniti 12 zimepatikana kutokana na zoezi hilo. Picha na Mohamed Hamad Chemba

Muktasari:

  • Wachangia uniti 12 walenga kuokoa maisha ya mama na mtoto, ambao wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama wanapofika hospitalini.

Kiteto. Mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga SC katika Kijiji cha Olboloti, wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, wamechangia damu salama uniti 12 kwa lengo la kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto ambao mara nyingi hupoteza maisha kwa kukosa damu

Wagizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumatano Novemba 15, 2023; wamesema kuwa hiyo ni sehemu ya fura kwa timu yao kufanya vizuri na kwamba hawana budi kuokoa maisha ya watu kwa kuchangia damu salama.

"Nimeamua kuchangia damu salama kwa sababu jamii yetu ina uhitaji mkubwa sana wa damu sio kituo hiki tu Afya na sehemu zingine na kila siku damu inahitajika kuna wanaopoteza maisha kwa kukosa damu"Karent Makanga Mshabiki  

Kwa upande wake Mariam Ramadhani shabiki wa Simba amesema tukio lililofanywa na mashabiki wa Yanga linapaswa kuigwa kwani linalenga kuokoa maisha ya watu

"Kwa tukio hili leo timu ya wananchi Yanga hata mimi mnyama hili ni tukio zuri sana la kuiga na ambalo nimeliunga mkononi... kubwa na ambalo ni muhimu ni kuokoa maisha ya watu kwa kuchangia damu salama,” amesema.

"Tuko kwaajili ya wananchi unachangia ulichonacho kama huna hela kweli hata damu huna? Hapana tunachangie damu ili isaidie watu wenye mahitaji," amesema khalibu Mgaya Shabiki wa Yanga. 

Kituo cha afya Mrijo imeelezwa kilikuwa na changamoto ya kupata damu salama haswa kwa ajili ya mama na watoto ambapo kwa wanafanya operesheni zaidi ya tano hivyo damu inahitajika 

"Kwa wiki tunafanya operesheni zaidi ya tano hivyo tumekuwa na uhaba mkubwa wa damu salama kusaidia mama wajawazito na watoto haswa wanapojifungua na kukosa damu...uhitaji wa damu salama hapa Mrijo ni mkubwa sana"amesema Daktari Sande Omari  

Kufuatia tukio hili Mwenyekiti wa kijiji cha Mrijochini anaonyesha kuguswa na mashabiki hao wa Yanga na kuwataka makundi mengine kuiga

"Tujifunze mambo haya ya kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa ni jambo ambalo dini zote zimeelekeza kuna ibada kubwa nq ni faraja kufariji wagonjwa ba kutoa misaada kama hii" Bashiru Mohamed