Wasomi wasioona wakumbukwa

Mwanafunzi wa fani ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ellis Lazaro, akikabidhiwa kifaa cha teknolojia cha watu wasioona na mratibu wa mradi wa elimu kwa watu wasioona nchini, Masamu Rumisha. Picha na Fina Lyimo

Muktasari:

  • Wanafunzi hao wakada mbalimbali wamepewa kifaa hicho pamoja na elimu ya namna ya kukitumia ambapo kwa wale watakao kwenda kufundisha kitarahisha kuandaa nyezo za kufundisha wanafunzi

Moshi. Wanafunzi wasioona 20 kutoka vyuo vikuu vitano nchini, wamepewa vifaa saidizi vya kuwawezasha kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa, vyenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni, kutoka Shirika la Kimataifa la Siloam lenye makazi yake nchini Korea ya Kusini.

 Wanafunzi hao kutoka wakada mbalimbali wamepewa vifaa hivyo pamoja na elimu ya namna ya kukitumia ambapo kwa wale watakao kwenda kufundisha vitarahisha kuandaa nyezo za kufundisha wanafunzi

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa  hivyo kwa Wanafunzi 20 kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini  mratibu wa mradi wa kuboresha elimu kwa wanafunzi wasioona nchini,  Rumisha Masamu, amesema kifaa hicho kina kila huduma ambayo mwanafunzi wa chuo anahitaji.

Amesema pia kifaa hicho kinafanya kazi zinafanywa na kompyuta mpakato na kwamba hicho ni kwaajili wa wanafunzi wasioona, kitarahisha kubeba nyenzo nyingi na kwa urahisi.

“Vifaa hivi vina njia mbili za matumizi, moja ni kupitia kusikiliza, wakati nyingine ni inatokana na kuvigisa, ni vifaa ambavyo vinabebeka na pia mtumiaji anaweza anaweza akapakuwa vitu mbalimbali kwenye mitandao ambapo vinarahisisha kazi na kuondoa tegemezi," amesema Masamu.

Aidha amesema vifaa hivyo ni vya gharama kwani kimoja kinagarimu zaidi ya Sh10 milioni na kuomba serikali ione namna ya kusaidia katika uwekezaji wa vifaa hivyo Wanafunzi wasioona.

Ellis Lazaro, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema kompyuta hizo mpakato kwa watu wasioona zitarahisisha kupata nyezo mbalimbali za masomo na hivyo kuondoa tegemezi

"Kifaa hicho tumefundishwa namna ya kukitumi na kitatusaidia sana wakati wa kufundisha na wakati wa kutafuta nyenzo mbalimbali kwenye mitandao pia kinatuondolea kuwa tegemezi wakati wa masomo" amesema Ellis

Kwa upande wake Innocent Shirima, amesema kutokana na fani ya uandishi wa habari ambayo anasemea kifaa hicho kitamsaidia kuandaa vipindi na makala mbalimbali bila kumtegemea mtu yeyote.