Watano wahofiwa kufariki ajali ya Coaster, lori Mikumi


Muktasari:

  • Mwananchi ilipomtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama amesema yuko njiani kuelekea eneo la ajali na atatoa taarifa kamili ya ajali hiyo.

Mikumi. Watu watano wanahofiwa kufariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari dogo aina ya Coaster iliyokuwa ikitokea mkoani Mbeya ikigongana na lori katika eneo la Iyovi Tarafa ya Mikumi mkoani Morogoro.

 Inadaiwa kuwa ajali hiyo imetokea asubuhi katika eneo hilo na wanaodaiwa kufariki na majeruhiwa kupelekwa Hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo Mikumi Wilaya ya Kilosa.

Mwananchi imezungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Alex Mkama ambaye amesema yuko njiani kuelekea eneo la ajali.

Mmoja wa askari wa usalama barabara aliyezungumza na Mwandishi wa Mwananchi kwa sharti la kutotajwa jina lake kwani yeye si msemaji wa Polisi amesema wamefika eneo la tukio na wanaendelea na uokoaji wa majeruhi.


Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi.