Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania wasisitizwa kutumia teknolojia za kifedha kuokoa muda

Mkurugenzi wawateja binafsi na wafanyabiashara wadogo na wakati wa Benki ya  (TCB), Lilian Mtali (kushoto) na Afisa Mkuu wa Huduma za kidigitali na Ubunifu Benki ya (TCB) Jesse Jackson (kulia) wakizindua kampeni ya  kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kufanya miamala mara kwa mara,halfa iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • Faida mojawapo ya kufanya miamala na huduma za kibenki kidijitali ni kuokoa muda, usalama, kujifunza biashara na ujuzi mbalimbali.

Dar es Salaam. Ili kuokoa muda wa kwenda benki, kuhakikisha usalama pamoja na kukuza uchumi kupitia  'Cashless economy', Watanzania wamesisitizwa kutumia njia za kidijitali katika huduma za kibenki ikiwemo kufanya miamala.

Faida hizo zimewekwa bayana na Benki ya Biashara Tanzania (TCB), ambayo inasisitiza matumizi ya kidijitali kwa wafanyabiashara, wateja na Watanzania kwa ujumla.

Akizungumzia hilo leo Ijumaa Aprili 25, 2025 Mkurugenzi wa wateja binafsi, wadogo na wa kati wa Benki ya TCB, Lilian Mtali amesema huduma za kibenki kwa sasa zinapaswa kufanyika kidijitali kwakuwa inarahisisha hata biashara, foleni hivyo kuokoa muda.

"Ukifanya miamala kidijitali utaona na fursa nyingine kwenye simu yako itakufungua zaidi kimawazo, utajifunza maarifa mapya kwenye biashara yako, kama ni mwanafunzi utajifunza hata teknolojia za kifedha 'Fintech," amesema.

Katika kuhamasisha matumizi hayo TCB imekuja na kampeni ya zawadi ya gari, pikipiki, Bajaji na simu kwa watakaotumia njia za kidijitali ikiwemo miamala kupitia huduma ya kibenki mtandao, popote Visa Card, Lipa popote.

Kampeni hiyo 'Toboa Kidijitali' kujishindia zawadi ya kila mwezi itakayofanyika kwa muda wa miezi minne iliyozinduliwa leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam inatajwa kuchochea matumizi ya dijitali katika huduma za kibenki

Aidha, amesema kampeni ya Toboa Kidijitali yenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni ni sehemu ya kurudisha kwa jamii, kurudisha kwa wafanyabiashara na wateja wanaofanya miamala na biashara kidijitali.

"Ukienda benki za nchi za wenzetu utaweza kuhisi benki zao hazina watu kwakuwa watu wanafanyia miamala dijitali wakiwa kazini au nyumbani ili kutenga thamani ya muda kwasababu muda ni pesa," amesema.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Huduma za kidigitali na Ubunifu Benki ya TCB, Jesse Jackson amesema huduma za kidijitali zinaletwa na mageuzi makubwa sekta ya kibenki yaliyopo sasa.

"Mwaka 2020 miamala ya kidijitali ilifanyika milioni 14 lakini takwimu zinaonesha hadi mwaka 2024 imeongezeka hadi milioni 21 sawa na ongezeko la asilimia 45," amebainisha.

Amesema huduma za kidijitali zina usalama na gharama nafuu sambamba na kuokoa muda kwa kufanya muda wowote mahali popote.

Aidha ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania BoT), kwa kutengeneza mazingira bora ya uwepo wa majukwaa ya kidijitali kwenye huduma za kifedha katika Benki za Tanzania.

Lakini amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa kuja na kampeni za kuwahamasisha watu zaidi katika matumizi hayo. Kwani kwa sasa asilimia 90 ya miamala Tanzania bado inafanyika kwa taslimu.