Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wa familia moja wafa wakiwa wamelala

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Watu watatu wa familia moja akiwamo mama mjamzito wamefariki dunia baada ya gema la udongo kuporomoka na kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe.


Songwe. Watu watatu wa familia moja akiwamo mama mjamzito wamefariki dunia baada ya gema la udongo kuporomoka na kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 28, 2022 katika Kitongoji cha Mijuni Kata ya Sange wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje (DC), Anna Gidarya amethibitisha tukio hilo na kwamba Serikali inaendelea kufuatilia.

Watu walioshuhudia wamesema waliofariki ni mume, mkewe ambaye alikuwa mjamzito pamoja na mtoto wao.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Sange, Elina Mbwilla amewataja waliofariki kuwa ni Lazaro Shibanda (25), Rozalia Kijalo (22) na mtoto Ayubu Shibanda mwenye umri wa miaka minne.

Amesema wananchi walikusanyika alfajiri na kufukua udongo na hatimaye kuwakuta wakiwa wamefariki.

Mtendaji huyo amesema aliwasiliana na Polisi ambao walikuwa njiani kuelekea eneo la tukio licha ya mvua kuendelea kunyesha.