Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto 637,720 kuchanjwa polio Kagera

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk Isesanda Kaniki akiongea na wajumbe mbalimbali wakati wa uzinduzi wa chanjo ya polio leo Alhamisi Aprili 14, 2022.

Muktasari:

Watoto 637,720 mkoani Kagera wanatarajiwa kupata chanjo ya polio ili kuwaepusha na athari ya ugonjwa huo unaoweza kusababisha kupooza baadhi ya viungo vya mwili.

Bukoba. Watoto 637,720 mkoani Kagera wanatarajiwa kupata chanjo ya polio ili kuwaepusha na athari ya ugonjwa huo unaoweza kusababisha kupooza baadhi ya viungo vya mwili.

Hayo yamesemawa leo Alhamisi Aprili 14, 2022 Msimamizi wa Taifa chanjo ya polio mkoani humo Regina Joseph wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo hiyo.

"Baada ya kupata taarifa kwamba nchi jirani ya Malawi ina mgonjwa mmoja  wa polio tumeanza kuchukua hatua kwa kuanza kampeni ya kulinda watoto wasiathiriwe na ugonjwa huo  na mikoa iliyopakana kama Songwe, Ruvuma, Njombe na Mbeya kwa kuchanja watoto wa umri wa miaka sifuri hadi mitano" amesema Regina

Ofisa Afya Mkoa wa Kagera, Zabron Segelu amesema kuwa kirusi cha polio kinasababisha kupooza baadhi ya viongo muhimu vya mwili kama miguu, mikono na mtoto kushindwa kutembea.

Amesema njia inayotumika kuingia virus hivyo kwenye mwili ni sehemu za mdomo, chakula ambacho kimechafuliwa na kama mtoto atakula au kuchezea mazingira hayo yenye kirusi hicho.

"Njia nyingine ni endapo mtoto amejisaidia eneo la wazi na mtoto mwingine akaingia au akachezea hapo lazima atapata kwani virus vinakaaa tumboni na hutolewa kwa njia ya kinyesi" amesema Segelu

Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera, Isesanda Kaniki amesema tayari mkoa umeanza kufanya mafunzo kwa wataalam ngazi ya mkoa ikiwa ni pamoja na kujadili jinsi ya kuyafikia maeneo yote.

Amesema chanjo hiyo itaendelea kutolewa kwenye hospitali, vituo Afya na zahanati hata kwa watoto watakao zaliwa watakuwa wanapata matone.