Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto watatu wa familia moja wateketea kwa moto Rombo

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Muktasari:

  • Watoto watatu wa familia moja ambao walikuwa wamelala chumba kimoja wameteketea kwa moto katika kijiji cha Samanga, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuungua moto.

Rombo. Watoto watatu wa familia moja waliokuwa  wamelala chumba kimoja wameteketea kwa moto katika kijiji cha Samanga, Kata ya Kirongo Samanga, wilayani hapa, mkoani Kilimanjaro baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuungua moto.

Watoto hao waliteketea  kwa moto alfajiri ya kuamkia leo Jumamosi, Desemba 16, 2023 wakati wazazi wao wakiwa wametoka kwenda kwenye utafutaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na  waliofariki dunia ni Oseline Laswai (9) mwanafunzi wa darasa la nne, Jolin Laswai (6) mwanafunzi wa darasa la kwanza, waliokuwa  wakisoma Shule ya Msingi Baraka pamoja na mdogo wao Anna Laswai (3).

"Leo iliungua moto nyumba iliyojengwa kwa mbao na kusababisha vifo vya watoto watatu ambao ni wakazi wa kijiji cha Samanga.

"Wakati tukio linatokea wazazi wa watoto hawa walikuwa wamekwishatoka kuelekea kwenye shughuli zao za kujipatia kipato majira ya saa 10:00 alfajiri," amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na miili ya watoto hao imehifadhiwa katika kituo cha afya Karume.