Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 24 wakamatwa wakizingira kituo cha polisi Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi

Muktasari:

Polisi mkoani Songwe wanawashikilia watu 24 wa Kijiji cha Chang'ombe wilayani Songwe kwa tuhuma za kuzingira kituo cha polisi Galula.

Songwe. Polisi mkoani Songwe wanawashikilia watu 24 wa Kijiji cha Chang'ombe wilayani Songwe kwa tuhuma za kuzingira kituo cha polisi Galula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amesema watu hao walivamia kituo wakishinikiza kurejeshewa mikoba ya waganga wa jadi (lambalamba) iliyokamatwa na askari wa kituo hicho.

Amesema watu hao walikizingira kituo hicho Novemba 22, 2021 alfajiri baada ya askari kuzuia kazi za lambalamba wanaowadhalilisha watu wakiwatuhumu ni wachawi.

Amesema kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji na watu wengine 23 wanashikiriwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba akiwa Mji Mdogo wa Mlowo aliwataka wakazi wa mkoa huo kuachana na wapiga ramli chonganishi wakiwamo lambalamba.