Watumia vyandarua kufugia kuku badadala kujikinga na mbu

Muktasari:

  • Kutokuwepo kwa uelewa wa matumizi ya vyandarua kumesababisha baadhi ya wananchi kutumia vyandarua kufugia mifugo badala ya kujkikingia na mbu na hivyo kuongeza kasi ya ugonjwa wa malaria.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa licha ya kuwepo kwa kampeni za matumizi ya chandarua ili kujikinga na ugonjwa wa malaria, bado ya wanawake wajawazito na wanyonyeshao kutoelewa njia hizo na hivyo kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa.


Sababu hizo na nyingine zimesababisha Taasisi ya Doris Mollell ikishirikiana na Shirika la Utafiti na Tiba Barani Afrika (Amref) kutoa elimu ya umuhimu wa kijikinga na malaria kwa wanawake wajawazito na wenye watoto hasa wakati huu ambao kuna maambukizi ya Ukivo-19.


Akizungumza leo Januari 14 kuhusu mafunzo hayo yaliyowafikia zaidi ya wanawake 300 katika mikoa ya Simiyu na Kagera, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Doris Mollell amesema katika ziara hiyo wamegundua kuwa baadhi ya maeneo matumizi ya vyandarau sio kipaumbele na badala yake wanawake hutumia kwa ajili ya kufungia kuku na mbwa.

"Serikali imefanya kampeni kubwa na kuhamaisha wanawake wajawazito na wenye watoto wadogo kuhakikisha wanalala kwenye vyandarau kwa ajili ya kujikinga na malaria, lakini bado kuna changamoto kadhaa mfano Kuna baadhi ya maeneo wanaume ndio hulala kwenye vyandarau," amesema Mollel.


Amesema wanawake wanapotoka kliniki na vyandarua wanaume huvichukua na kuvitumia kwenye kazi nyingine na kupiteza lengo lililokusudiwa la kudhibiti malaria.


“Bado nchi ipo kwenye wimbi la uwepo wa Uvik-19 kwa hiyo wanawake wajawazito na wanaonyonyesha hawanabudi kujikinga na maambukizi ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa malaria,” amesema.