Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumishi 16 Dar watuhumiwa ‘upigaji’ Sh8.9 bilioni

File Photo

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili watumishi 16 wakiwemo wahasibu wanaokabiliwa na mashtaka 143 umedai upelelezi umekamilika.

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili watumishi 16 wakiwemo wahasibu wa Jiji la Dar es Salaam umedai upelelezi umekamilika wanaandaa taarifa kwa ajili ya kuituma Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 143 likiwemo la kuisababishia hasara jiji hilo zaidi ya Sh8.9 bilioni.

Wakili Serikali, Pendo Temu alidai mbele ya Hakimu Mkazi kisutu Pamela Mazengo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wanaandaa taarifa kwa ajili ya kuituma mahakama kuu hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kutajwa.

"Upelelezi umekamilika wapo kwenye mchakato wa kuandaa taarifa kwa ajili ya kuituma Mahakama Kuu," amedai Temu.

Washtakiwa hao ni Tulusubya Kamalamo, James Bangi ambao ni wahazini,  Mohamed Khars, Abdallah Mlwale na Deogratias Lutatuza na Alinanuswe Mwakasumbe ni wahasibu pamoja na Judica Ngowo ambaye ni karani wa fedha.

Wengine ni Febronia Nagwa, Glory Eugen, Said Bakari, Josephine Sandewa, Dorica Gwihala, Jesca Lugonzibwa, Patrick Chibwana ambao ni wahasibu, Patrick Chubwana Ofisa Afya , Ally Baruan meneja na Khalid  Nyakamande Afisa mtendaji wa mtaa.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa  Julai Mosi, 2019 na Juni 30, 2021 jijini Dar es Salaam washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha na kujipatia kiasi cha  Sh8.9 bilioni mali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 11, 2023 kwa ajili ya kutajwa.