Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawakilishi saba wa LBL mbaroni Geita

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Adam Maro akizungumza na waandishi wa habari.

Muktasari:

  • Uchunguzi umebaini umebaini kampuni ya LBL haina nyaraka halali za kufanya biashara za fedha wala kuchangisha wananchi na pia hana vibali kutoka BOT.

Geita. Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu saba ambao ni wawakilishi wa Kampuni ya Leo Beneth London (LBL) kwa tuhuma za kuendesha biashara ya fedha mtandaoni bila kuwa na kibali cha Benki Kuu ya Tanzania.

Kaimu Kamanda Maro amesema watu hao waliopo mji mdogo wa Katoro wamekuwa wakiwatoza wananchi fedha kati ya Sh50,000 hadi 540,000, wakiwataka watazame video fupi inayotangaza faida watakayokuwa wakipata pindi wakijiunga na kampuni hiyo, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Waliokamatwa ni Juma Nicholaus, Stefano Kafulila, Ramadhan Masood, Alfred Matiba, Rebeca Mazabali, Elizabeth Zacharia na Athuman Masunga.

Jeshi hilo, pia, limekamata vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika kutekeleza uhalifu huo ambavyo ni kompyuta moja, simu janja nane, laini za simu 21, notebook yenye majina na nyaraka mbalimbali ambazo zinakumbukumbu za wateja.

Amesema uchunguzi umebaini umebaini kampuni ya LBL haina nyaraka halali za kufanya biashara za fedha wala kuchangisha wananchi na pia hana vibali kutoka BOT kwa ajili ya kufanya biashara hiyo na kwamba watu hao wanaendelea kushikiliwa kwa taratibu za kufikishwa mahakamani.