Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawatuhumu viongozi wao kushindwa kusimamia maendeleo

Mbunge wa Solwa, Ahmed Salum akizungumza na wakazi wa Kata ya Salawe kwenye Mkutano wa hadhara.

Muktasari:

Wananchi wa Kata ya Salawe mkoani Shinyanga wamewatuhumu viongozi wa Kata hiyo kuwabambikia kesi na kushindwa kusimamia utekelezaji wa miradi katika Kata hiyo.

Shinyanga. Wakazi wa Kata ya Salawe Halmashauri ya Shinyanga wamewatuhumu baadhi ya viongozi wa Vitongoji na Kata kuwabambikiza kesi na kushindwa kusimamia shughuli za maendeleo ukiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Salawe.

Wametoa malalamiko hayo Julai 28, 2023 kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mangu ulioitishwa na Mbunge wa Solwa, Ahmed Salum ili kusikiliza kero zao, wakidai wamechoka kunyanyaswa na baadhi ya viongozi kwa kushirikiana na jeshi la jadi (sungusungu).

Mkazi wa kijiji hicho, Edmund Nkonya amesema viongozi waliowachagua kusaidia kufikisha kero zao katika ngazi ya Wilaya wao ndiyo wamegeuka na kuanza kubambikiza kesi wananchi badala ya kuwasaidia.

“Hatuna maendeleo kwenye Kata yetu wananchi tunachangishwa michango kwa ajili ya maendeleo yetu lakini mwisho wa siku hakuna kinachofanyika fedha zinaishia mfukoni kwa baadhi ya viongozi hii haikubaliki hatuwataki viongozi hawa," amesema Nkonya

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Songambele, Shija Mahega amesema wanaumizwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wao.

Mei 20, 2022 taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kuanza uchunguzi katika ujenzi wa Kituo cha afya Salawe kutokana na kulalamikiwa na wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mbunge wa Solwa,  Ahmed Salum amesema ndani ya Kata ya Salawe kuna viongozi ambao ni mchwa wanakula fedha za Serikali za miradi ya maendeleo na kukwamisha wananchi kupata huduma mapema.

Amesema Serikali inatoa fedha nyingi lakini usimamizi wa fedha hizo hakuna na matokeo yake miradi inaanzishwa na haikamiliki kama ilivyokusudiwa kikiwemo kituo cha afya Salawe ambacho hakijakamilika licha ya Serikali kutoa fedha zaidi ya Sh1 bilioni.

“Ninapambana kutafuta fedha kwa wadau mbalimbali na kuzungumza na viongozi wa Wizara lakini fedha zinapoletwa kwenye Kata usimamizi unakuwa shida viongozi tunaowaamini wanakuwa mchwa," amesema

Amesema viongozi wote watakaobainika kuhusika kutafuna fedha za ujenzi wa kituo hicho lazima wachukuliwe hatua na kurejesha fedha walizokula akidai fedha iliyotolewa ilikuwa inaweza kujenga vituo viwili vya afya lakini hata kilichopo hakijakamilika.