Wawili kortini kwa tuhuma za kujaribu kumuua mtoto wa miaka sita

Mshtakiwa Clemensia Milembe(19) aliyesimama pembeni ya askari polisi katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kujaribu kuua.
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa ndani, Clemensia Milembe (19) na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni,wakikabiliwa na shitaka moja la kujaribu kuua.
Mbali na Milembe, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ni Elizabeth Makori(38) maarufu mama Brayan, mkazi wa Goba.
Washtakiwa hao wakabailiwa na kesi ya kujaribu kuua kinyume na kifungo 211 kifungu kidogo (a) cha Sheria ya Adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Washtakiwa wote ambao ni wakazi wa Goba, wamefikishwa mahakamani hapo leo Agosti 15, 2024 na kusomewa shitaka hilo na wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalila
Wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu amedai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wanakabiliwa kesi ya kujaribu kuu namba 22964/2024
Akiwasomea shitaka lao, wakili Kamungu amedai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 15, 2024 katika eneo la Goba Kizundi iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni.
Inadaiwa siku ya tukio, washtakiwa kwa pamoja walijaribu kusababisha kifo kwa mtoto Maliki Kitumbi mwenye umri wa miaka sita.
Endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi