Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi watakiwa kuhimiza watoto, familia kujifunza maadili ya dini

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye ibada ya  Eid el Adh'haa iliyofanyika Msikiti wa Nnaiim uliopo Vibaoni wilayani Handeni mkoani Tanga leo Alhamis Juni 29, 2023. Picha na Rajabu Athumani

Muktasari:

  • Sikukuu ya Eid el Adh’haa ni swala inayofanyika baada ya kukamilika nguzo ya tano ya dini ya Kiislamu ya kwenda Hijja kwa wenye uwezo.

Handeni. Waumini wa dini ya Kiislamu hasa wazazi wametakiwa kujifunza maadili ya dini ili kuweza kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwenye familia zao na jamii kwa ujumla.

Akihutubia waumini wa dini hiyo waliojitokeza katika swala ya Eid el Adh’haa iliyofanyika Msikiti wa Nnaiim wilayani Handeni mkoani Tanga leo Alhamisi Juni 29, 2023 Msoma hotuba katika swala hiyo, Farhan Kidelengwe amesema kuna wazazi hawajasoma dini na wala watoto wao hivyo kuwa chanzo cha kuharibika maadili.

Amesema wanaume ndio wasimamizi wakuu wa familia kama mwongozo wa dini unavyosema, lakini wapo baadhi yao wanakwepa jukumu hilo na kuwaachia wanawake, pekee hali ambayo ndio chanzo kikubwa kuharibika maadili kwenye jamii.

"Wanaume sisi ndio viongozi wa familia lakini wapo wengine wanashindwa kusimamia familia zao, mtoto anatoka ndani amevaa nguo za ajabu, lugha za matusi lakini hakuna hatua zinachukuliwa hili ni tatizo na tunatakiwa wanaume kuwajibika," amesema Farhan.

Imamu msikiti wa Nnaiim wa Kata ya Vibaoni, Kombo Nkucha amesema familia nyingi wazazi hawafuatilii masuala ya dini na badala yake wamejikita kwenye kufuatilia mipira na starehe nyingine jambo ambalo hata watoto wanaiga kile wazazi wao wachokifanya.

Amesema mzazi anafuatilia mambo ya mpira muda wote tena kwa gharama yoyote ile lakini suala la kujifunza dini na maadili yake muda huo hana, kitendo ambacho na familia nayo inaangalia mwenendo wa wazazi na kuiga yale wanayofanya," amesema sheikh Nkucha

Muumini wa dini hiyo, Amir Mohamed amesema chanzo kingine cha kuharibika maadili ni wazazi kuogopa kuongea na watoto wao kuhusu maadili na mafundisho ya dini.