Waziri awaonya wanaoiba madini

Muktasari:
- Waziri wa Madini, Dotto Biteko ametoa onyo kwa wanaoiba madini na kuyauza bila utaratibu kwani Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria.
Bukoba. Waziri wa Madini, Dotto Biteko ametoa onyo kwa wanaoiba madini na kuyauza bila utaratibu kwani Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria.
Biteko ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 5, 2022 katika mkutano wa kamati ya ufuatiliaji wa madini nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) unaoendelea mkoani Kagera ambao umeanza April 04 na utamalizika Aprili 8.
Amesema kwamba ICGLR kazi yake kubwa ni kudhibiti madini yanayotoroshwa na kuuzwa nje ya mfumo.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaonya na kuwaambia kwamba Serikali haitamfumbia macho mtu hata mmoja ambaye haendi kuchimba badala yake anasubili wenzie wachimbe aende kuwaibia hatutakubali na wale ambao watajihusisha na vitendo hivyo wako wengi wamekamatwa na tutaendelea na zoezi hili la kukamata.
“Nitoe onyo kwa wanaohusika, kama wanafikiri wanaweza kujaribu wawaulize waliojaribu kwa sababu hakuna mtu atakayefanikiwa katika hili na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kila mtu anayefanya kazi yake apate manufaa kwenye kazi yake siyo mtu mwingine aliyekaa nyumbani anasubili kwenda kuwaibia wenzake, hili halitakubalika” amesema Biteko.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji maswala ya madini nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) kutoka nchi ya Kidemokrasia ya Congo, David Ngoy amesema kuwa kazi wanayoifanya (ICGLR) inapunguza ujambazi