Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Jafo aagiza waliovamia mto Ruaha kuondolewa

Muonekano wa hali ya mto Ruaha Mkuu katika daraja la Ibuguziwa ambao umekauka kutokana na shughuli za kibinadamu za kilimo na mifugo kando ya vyanzo vya maji na ndani ya hufadhi ya Ruaha. Picha na Berdina Majinge

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo ameagiza wananchi waliovamia vyanzo vya maji ikiwamo katika Hifadhi ya Ruaha kuondolewa katika maeneo hayo.

Iringa. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo ameagiza wananchi waliovamia vyanzo vya maji ikiwamo katika Hifadhi ya Ruaha kuondolewa katika maeneo hayo.

Amezitaka mamlaka za mabonde na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kusimamia sheria ya maji ya mwaka 2022 ili kunusuru mto Ruaha Mkuu ambao kwa sasa umekauka.


Waziri Jafo ametoa maagizo hayo wakati wa kikao cha mawaziri nane, wakuu wa mikoa na wataalamu kilichofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Amesema viongozi hao wamekuwa mashahidi kwani hali ya hewa ya mwaka huu imebadilika kiwango cha mvua ambacho walitarajia kinyeshe hivi karibuni hadi sasa bado hali ni ya ukame.

“Kukosekana kwa maji katika hifadhi ya Ruaha kutasababisha wanyama, samaki kufa kutokana na kiwango cha oksijeni kupotea katika maji yanayowafanya waishi, hivyo naziagiza mamlaka husika kuanza kuchukua hatua kwa wote wanaochepusha maji kinyume cha sheria, na kuendelea kusimamia wale wote waliopata kibali kama vinatumika ipasavyo” amesema Waziri Jafo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


“Bodi ya mabonde yote zihakikishe zinasimamia sheria ya maji iliyoainishwa mwaka 2022 hii imetuelekeza ya kwamba wale wanaochepusha maji kinyume na utaratibu waweze kuchukuliwa sheria kwa mujibu wa sheria ya maji”


Amesema mto Ruaha mara nyingi unatiririsha maji mwaka mzima lakini inashangaza mwaka huu mto huo umekauka.


“Tumejionea wenyewe katika eneo la darajani sehemu yenye kina kirefu kati ya maeneo mengi tumeona hata maji kidogo yaliyobakia pale yale vidimwi hata viboko wanaoishi eneo hilo hatujui hatima yao endapo mvua isiponyesha ndani ya wiki mbili zijazo.

“Wale wote waliovamia vyanzo vya maji waondoke haraka iwezekanavyo mara baada ya kikao cha mawaziri, wakuu wa mikoa na wataalamu kimeelekeza ya kwamba wale wote wanaovamia vyanzo vya maji na kuleta uhalibifu mkubwa waondoke haraka”.


Pia, Waziri Jafo ameagiza shughuli ya utambuzi wa mifugo kwenda kufanyiwa kazi kwa sababu wanashaka na mifugo mingine inawezekana sio mali ya nchi hii inatoka nje ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amesema wameshuhudia mto Ruaha Mkuu umeanza kukauka na kuwataka Watanzania kutunza na kuendelea maliasili walizo nazo.

“Nawaombeni sana tushirikiane kutunza na kuendeleza hifadhi zetu katika misitu kuna vyanzo vya maji muhimu vinavyoweza kutumika kwa idadi ya watanzania takribani million 61, maji haya pia yanasaidia wanyamapori wetu na serikali kupata mapato”amesema Dk Pindi


Kamishna wa uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema amesema kuwa changamoto kubwa katika hifadhi ya Ruaha ni kukauka kwa maji katika mto Ruaha Mkuu ambapo inasababishwa na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kando ya vyanzo hivyo.