Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Makamba aanza kuvalia njuga nishati safi ya kupikia

Waziri wa Nishati, January Makamba akimtizama namna kikundi cha kusindika na kuchakata samaki na dagaa cha Kusama cha Musoma Mjini kinachotumia kuni katika utekelezaji wa shughuli zake.Katika ziara hiyo Makamba aliahidi kuwafungia mfumo wa majiko wa gesi ili kufanya shughuli zao kwa ufanisi

Muktasari:

Waziri wa Nishati nchini Tanzania, January Makamba ameamua kulivalia njuga suala la nishati ya kupikia ili kuboresha afya na maisha ya Watanzania hasa wanaoishi katika vijijini.

Musoma.  Serikali ya Tanzania imeanza kuvalia njuga upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ili kuboresha maisha na afya za Watanzania hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

 Kwa sasa wakazi wengi wa mijini wanapata kwa urahisi nishati hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba leo Jumatatu, Julai 11, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa Musoma na Butiama mkoani Mara kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya mikoa 14 inayolenga kusikiliza kero na maoni ya wananchi.

Amesema wamedhalimilia kuifanya sekta ya nishati hasa ya kupikia kwa sababu inagusa maisha ya watu wengi.

Waziri huyo amesema Serikali imeamua kutoa msukumo katika nishati ya kupikia ili kuboresha afya za wananchi ambao wakivuta moshi unatokana na kuni au mkaa wana hatari ya kupata changamoto ya mfumo wa upumuaji, macho kuwa rangi nyekundu pamoja kichomi.

"Tumelishikilia bango suala hili kuanzia sasa tunataka kuondoa changamoto kwa wananchi wa vijijini wanaotumia nishati ya kuni na mkaa. Wanaopikia kuni wanapata madhara mbalimbali tumetoka hospitali tumeelezwa haya," amesema Makamba.

Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Dk Mary Mahenga amemweleza Waziri Makamba kuwa moshi unaotokana matumizi ya kuni na mkaa una madhara mbalimbali katika mwili wa binadamu ikiwemo kusababisha watoto njiti.

Katika kuhakikisha wamedhalimilia hiyo, Makamba alimkabidhi Teleza Stephano mtungi wa gesi, akimtaka kuachana na matumizi ya kuni anayatumia kwa sasa.

Amehakikishia mtungi huo ukiisha atajaziwa huku akifundishwa namna ya kuutumia ili kuachana matumizi ya kuni.

Akizungumzia hatua hiyo, Teleza anayeishi eneo la Kisamwene wilayani Butiama ameshukuru Makamba kwa msaada huo akisema matumizi ya kuni katika kupikia yalikuwa yakimpa changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo macho kuuma kwa nyakati tofauti pamoja kifua kumbana.

Siyo Teleza pekee yake, bali Makamba aliwaahidi viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania ( UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwapa mtaji wa mitungi ya gesi 300 kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi kwa gharama nafuu ili waondokane na nishati chafu ya kupikia.

Pia, ametembelea na kuwapa mitungi ya gesi wanakikundi cha kuchakata na kusindika samaki cha Kusama, ili kuondokana na matumizi ya kuni katika shughuli zao za ukaangaji wa samaki na dagaa.


Katika hatua nyingine, Makamba aliwahakikisha wananchi wa Butiama walioomba umeme kupitia REA kuwa kuanzia wiki ijayo wataunganishia nishati hiyo, akisema kijiji kimoja na vitongoji vya wilaya hiyo vilivyobaki vitapata huduma hiyo.

Mbunge wa Butiama (CCM), Jumanne Sagini ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, amesema suala la umeme katika jimbo hilo lilizungumzwa kwa muda mrefu na anaishukuru wizara hiyo kwa kupeleka huduma hiyo wilayani humo.

Mikoa ambayo Waziri Makamba anaitembelea ni Mara, Mwanza, Kagera, Geita, Katavi, Tabora, Shinyanga, Songwe, Simiyu, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara.