Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Ndaki awataka wafugaji kubadili mbinu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza na wafugaji wa kata ya Nyololo na Maduma.

Muktasari:

  • Waziri wa Mifugo na Uvuvi awataka wafugaji kubadiki mbinu za ufugaji ili kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima.

Iringa. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wafugaji kubadili mbinu ya ufugaji kutoka ule wa asili ambao umekuwa kichocheo cha migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Waziri Ndaki amesema hayo leo Desemba 7, 2022 wilayani Mufindi wakati wa kukabidhi ng’ombe kwa wafugaji wanaonufaika na Mradi wa Animal Gift unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania katika Kata za Nyololo na Maduma mkoani Iringa.

Amesema serikali inatekeleza mpango wa mabadiliko ya sekta ya mifugo nchini ikiwemo kuhamilisha mifugo kwa kutumia mbegu chotara na kuacha kufuga ngombe wengi badala yake wapunguze idadi ya mifugo.

“Mwaka huu wa fedha tunataka tuhimishe ng’ombe 373,000 kwa nchi nzima ili hiyo mifugo badala ya kuzaa ng’ombe wa kienyeji izae ng’ombe machotara watakao kuwa na uzito mkubwa lakini watakaoweza kutoa maziwa mengi,” amesema.

“Tukiendelea kuwa na idadi ya mifuko tuliyonayo sasa hivi tutaendelea kuwa na migogoro isiyoisha kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi,” amesema.

Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la World Vission Tanzania, Dk Joseph Mayala amesema wanaotekeleza mradi huo kwa ufadhiri wa World Vision Marekani anaeleza changamoto za mradi huo.

Mayala amesema mradi huo unatarajiwa kutumia bajeti ya fedha za kitanzania bilioni 1.4 ambapo itahusisha kununua ng’ombe wa kisasa wa maziwa 300, nguruwe 600 na kuku 4,000 kwa kipindi chote cha mradi.

“Tunaomba serikali iruhusu madume bora 10 yaliyokusudiwa tunayoyahitaji katika mradi huu yanunuliwe katika mashamba ya serikali ili kuongeza uhakika wa ubora na ufanisi,” amesema.


Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wanasema pamoja na maandalizi ya kupanda nyasi kwa ajili ya malisho changamoto ni waliyonayo ni mbegu za malisho hayo.

“Tunaomba waweze kutusaidia kutokana na mazingira tunayoishi ni magumu tuna mashamba tumeandaa kwa ajili ya kupanda chakula cha ng’ombe. Tunaomba msaada serikali itusaidie mbegu kwa ajili ya kulishia mifugo yetu,” amesema Mgimba.

Akijibu ombi hilo Waziri Mashimba amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Word Vision itaende wizarani watawapewa mbegu na wawafundishe wafugaji ambao hawana uelewa wowote wa ufugaji wa kisasa ili waweze kuzilima na kuwanufaisha mifugo yao