Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri wa zamani afichua pengo lililopo uwezeshaji wa vijana wa kiume

Waziri wa zamani wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.

Muktasari:

  • Amesema uchache wa majukwaa ya kiuchumi na maadili kwa vijana wa kiume ikilinganishwa na wanawake kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea mmomonyoko wa maadili, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, jambo ambalo ni hatari kwa kundi hilo.

Kibaha. Waziri wa zamani wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ameeleza hatari inayowanyemelea vijana iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuwaanzishia majukwaa ya kuwaongezea fursa za kiuchumi na maadili.

Pia, amewataka wazazi kuongeza ushirikiano na Serikali katika kuwaongezea maarifa juu ya maadili mema na fursa za uchumi akieleza kuwa kundi hilo limeendelea kusahaulika ikilinganishwa na watoto wa kike.

Simba amebainishwa leo Juni 29, 2026 mjini Kibaha mkoani Pwani wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya Kikundi cha Super Woman 2017.

Amesema uchache wa majukwaa ya kiuchumi na maadili kwa vijana wa kiume ikilinganishwa na wanawake kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea mmomonyoko wa maadili, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, jambo ambalo ni hatari kwa kundi hilo.

Amesema Taifa haliwezi kufikia maendeleo endelevu ikiwa sehemu kubwa ya vijana wa kiume itaendelea kukosa mwelekeo wa kiuchumi na maadili.

Amesema changamoto za ukosefu wa ajira, mitaji, stadi za kazi na malezi bora zimewaacha baadhi ya vijana katika mazingira yanayowasukuma kujiingiza kwenye vitendo visivyokubalika, hivyo kuna ulazima wa jamii hasa akina mama kuweka mikakati madhubuti ya kuwainua vijana wa kiume.

“Vijana wa kiume wameendelea kusahaulika, umefika wakati akina mama tukae karibu na watoto wetu hao kuwapa mafunzo na mbinu pamoja na kutafuta fursa zinazowasaidia kupewa nafasi, kuaminiwa na kuwezeshwa,” amesema.

Amesema jukumu la kuwajenga vijana si la Serikali pekee, bali linahitaji ushiriki wa wazazi, wanawake na wadau wengine ili kuhakikisha vijana wanapata malezi bora, ushauri na fursa za kujitegemea.

“Wanawake mmeonyesha mfano mzuri wa kujipanga kupitia vikundi vyenu vya kiuchumi. Sasa uzoefu huo utumike pia kuwalea na kuwawezesha vijana wa kiume ili wajenge uchumi wao na kurejea kwenye misingi ya maadili mema. Tukiwainua vijana, tutakuwa tumeijenga familia, jamii na Taifa kwa ujumla,” amesema.

Awali, Mwenyekiti wa Kikundi cha Super Woman 2017, Bertha Kimambo amesema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia utaratibu wa kuweka akiba, kukopeshana na kusaidia makundi maalumu.

Amesema katika kipindi cha miaka 10, wanachama wengi wamefanikiwa kuanzisha na kupanua biashara, kuboresha maisha ya familia zao na kujijengea uwezo wa kifedha kutokana na mshikamano na nidhamu ya kuweka akiba.

Mmoja wa wanachama waanzilishi, Bety Msimbe amesema pamoja na mafanikio hayo bado wanakabiliwa na changamoto ya mtaji, lakini wameendelea kushirikiana na kusaidia jamii, huku wakipanga kuanzisha mradi wa pamoja utakaotoa ajira kwa wanawake na vijana.