Wikiendi ya Mbowe, Zitto

Muktasari:

Wanasiasa hao wa upinzani, kila mmoja akiwa mbali na mwenzake walijikuta wakikumbana na misukosuko iliyolihusisha Jeshi la Polisi.

Dar es Salaam. Jumapili iliyomalizika muda mfupi uliopita imehitimisha siku saba za wiki, lakini kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo , Zitto Kabwe haikukamilika walivyoitarajia.

 Wanasiasa hao wa upinzani, kila mmoja akiwa mbali na mwenzake walijikuta wakikumbana na misukosuko iliyolihusisha Jeshi la Polisi.

 Wakati Mbowe akishikiliwa kwa saa mbili na Polisi mjini Mwanza, Zitto alikuwa akisakwa na jeshi hilo, huku pia ikielezwa askari kanzu walikuwa wakimvizia katika ofisi za chama chake.