Wizara yatafuta wafadhili kulipia ada wanaoshindwa kuendelea vyuo

Saturday November 27 2021
wizarapic

By Robert Kakwesi

Tabora.  Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, ina mpango wa kushirikiana na Vyuo vya Afya binafsi kutafuta wafadhili kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wasio na uwezo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Dr Dorothy Gwajima katika mahafali ya Kwanza ya Chuo Cha Afya Cha St Maximilliancolbe mjini Tabora Leo.

Amesema Kuna changamoto kubwa kwa wanavyuo vya kati kutopata mikopo na kuwa wasio na uwezo ni lazima wasaidiwe kusoma.

"Inaumiza mwanafunzi kuishia njiani shauri ya kukosa ada katika masomo yake"Amesema

Dr Gwajima alikuwa akijibu ombo la Mkurugenzi wa Chuo hicho,Elizabeth Nkonyoka na mkuu wa Chuo,Nassoro Madende ambao walieleza masikito Yao kwa baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kwa ukosefu wa ada.

Walimuomba Waziri huyo kusaidia kuwatafuta wafadhili ili waweze kutoa mchango wao kwa kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kwa ukosefu wa ada.

Advertisement


Waziri Gwajima amesema wataongea na taasisi ya Dunia kwa vile wapo wasamari wema wanaoweza kusaidia na kuwa kama likiandikwa andiko wanaweza kutoa mchango wao kusaidia wanafunzi wanaokosa ada na kushindwa kuendelea na masomo.


Hata hivyo ametaka Ushirikiano kikiwamo chuo hicho katika kuandika maandiko ya kuomba kusaidiwa wanafunzi wanaokosa ada za kulipia masomo Yao.

Wanafunzi 37 wamehitimu katika chuo hicho katika mahafali hayo ya Kwanza na kutunukiwa stashahada ya Sayansi ya Famasi.


Advertisement