Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zaidi ya 1,000 waitwa kuanza kazi serikalini

Muktasari:

  • Watu zaidi ya 1,000 wameitwa kuanza kazi serikalini, baada ya kufaulu usaili uliofanyika kati ya Julai 21, mwaka jana hadi Juni 29, mwaka huu.

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imewaita kazini zaidi ya 1,074 waliofaulu usaili uliofanyika kati ya Julai 21, 2025 na Juni 29, 2026 na kuwapangia vituo vya kazi baadhi yao.

Wengine walioitwa kazini ni wale waliofanya usaili kati ya Julai 21, 2025 hadi Juni 24, mwaka huu.

Tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira leo, Jumanne Julai 21, 2026, pia linahusisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata za kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata barua zao za kupangiwa kazi kupitia akaunti zao za Ajira Portal.

Wasailiwa hao wametakiwa kuingia kwenye akaunti zao, kupakua na kuchapisha barua hizo kabla ya kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa.

Sekretarieti hiyo, imeeleza kuwa waajiriwa wapya wanapaswa kufika kwa waajiri wao ndani ya muda ulioainishwa kwenye barua za kupangiwa kazi.

Pia, wametakiwa kuwasilisha vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi za ajira.

Hatua hiyo, taarifa inasema inalenga kuthibitisha uhalali wa sifa za waombaji kabla ya kukamilisha taratibu za kuajiriwa katika utumishi wa umma.

Kwa upande mwingine, waombaji ambao majina yao hayajaonekana kwenye tangazo hilo wametakiwa kutambua kuwa hawakufaulu usaili au hawakupata nafasi za ajira zilizokuwa zikitangazwa.

Sekretarieti ya Ajira kupitia taarifa hiyo, imewahimiza waombaji hao kuendelea kufuatilia na kuomba nafasi nyingine za kazi zitakapotangazwa siku zijazo.