Zuma ahukumiwa kifungo cha miezi 15 jela
Muktasari:
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 jela aliyekuwa rais wa Taifa hilo, Jacob Zuma.
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miezi 15 jela aliyekuwa rais wa Taifa hilo, Jacob Zuma.
Ni baada ya kukutwa na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada ya kutoonekana katika kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.
Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama, Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo, aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.
Tangu alipojiuzulu mwaka 2018, Zuma amekuwa akifika mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi ambayo mara kadhaa ameyakanusha.