‘drones’ kusafirisha kwa haraka dawa za dharura
Muktasari:
- Kampuni ya Zipline kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamekubaliana kuanza majaribio ya kurusha ndege zisizo na rubani (Drones) kwa ajili ya kusambaza dawa kwenye vituo vinavyohitaji huduma za dharura vile vilivyoko katika maeneo ya vijijini na hospitali zisizofikika kwa urahisi.
Zahanati zilizopo katika maeneo ya Visiwa vya Ukerewe na yale mengine yasiyofikika kwa haraka kama ya Tewe, mkoani Tanga yenye miundombinu mibovu inayochangia Bohari ya Dawa (MSD) kushindwa kuikishaji dawa na vitendanishi hasa kwa huduma za dharura, sasa yamepatiwa mbadala.
Kampuni ya Zipline kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamekubaliana kuanza majaribio ya kurusha ndege zisizo na rubani (Drones) kwa ajili ya kusambaza dawa kwenye vituo vinavyohitaji huduma za dharura vile vilivyoko katika maeneo ya vijijini na hospitali zisizofikika kwa urahisi.
Uwapo wa teknolojia hiyo utawezesha kuokoa maisha ya wagonjwa, kwani sasa ndege hizo zitasambaza damu, chanjo na dawa muhimu ndani ya muda mfupi kwa vituo ambavyo ufikiwaje wake una changamoto.
Wakati Tanzania ikiingia katika teknolojia hii rahisi, tayari kampuni hiyo imeshaanza kusambaza damu kwa huduma za dharura nchini Rwanda, ambako tangu Oktoba 2016 mpaka Mei, mwaka huu, walikwishafanya safari 350 za mafanikio.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu anasema wakati wakianza utafiti wa majaribio ya huduma hiyo mapema mwakani, ndege hizo zitafanya kazi ili kuokoa maisha ya wagonjwa pamoja na gharama.
Anasema mkataba uliosainiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Zipline, yataanza rasmi kwa kuangalia jinsi ya kuitumia teknolojia hiyo ifikapo mwaka kesho.
Kabla ya kuanza huduma hiyo, Bwanakunu anasema watashirikiana na Ifakara Health Institute (IHI) ambao watafanya utafiti wa kuangalia uwezekano wa drones kufanya kazi Mkoani Dodoma, majaribio ambayo yatafanyika katika eneo la Chamwino na Mkoani Mwanza na baada ya mwaka mmoja wakipata matokeo chanya, usambazaji utaanza mara moja.
“kama tutapata matokeo chanya, tutazunguka mikoa mingine 10 ili kuwafikia zaidi ya watu milioni 10 wanaoishi katika maeneo yasiyofikika,” anasema Bwanakunu.
Anasema baada ya mwaka mmoja wanatarajiwa kutakuwa na maeneo manne tofauti ambayo ni Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Mkoa wa Tanga na maeneo ya Dodoma ambayo yatafanya kazi ya usambazaji rasmi.
Akizungumzia uratibu wa usambazaji wa dawa hizo namna utakavyoratibiwa, Bwanakunu anasema Bohari ya Dawa watakuwa na jukumu hilo na pindi vituo vitakavyotoa taarifa kuhusu huduma hizo za dharura, vitapokea meseji kwa njia ya simu ya mkononi kutoka MSD ikielezea mzigo uliotumwa.
“Vituo vitakuwa vinapokea kwa ujumbe wa simu kupitia simu zao za mkononi na huku itakuwa inadurufu nyaraka, kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuanza kuzungumza na kitengo cha damu salama kwa kuwa sisi hatusambazi damu lakini pia Tamisemi lakini mratibu mkubwa wa mradi huu ni MSD,” anasema.
Anafafanua kuwa ndege hizo ni maalum kwa ajili ya dharura na hazichukui mzigo mkubwa na zinakwenda kwa haraka na itakuwa na uwezo wa kufikisha mzigo kwa haraka ndani ya dakika 30 na ina uwezo wa kubeba uzito wa kilogram 1 mpaka moja unusu.
Bwanakunu anasema kutakuwa na ndege 30ambazo zitakuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 160 ambazo kwa anga ni umbali mrefu katika kila eneo na kwamba ndege za kituo kimoja zitakuwa na uwezo wa kufanya safari 2000 kwa siku.
“Januari mwakani tutaanza kazi, sisi tunatumia teknolojia hii kuokoa maisha ya binadamu na kupunguza gharama ndiyo hasa lengo letu kwenye mradi huu. Taarifa kuhusu wapi kuna tatizo tutapata kutoka kwenye vituo vya kutokea huduma za afya, kila kitu kitakuwa kimeunganishwa na mfumo wetu,” anasema.
Akizungumzia suala hilo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Mpoki Ulisubisya anasema MSD imekuwa ikipeleka huduma kwa vituo 5640 nchini lakini changamoto kubwa ni maeneo yasiyofikika kwa urahisi.
Anasema teknolojia hiyo ya ndege zisizo na rubani ambazo kiutaratibu zinatumika vitani Zipline wamekuja kutumia teknolojia hiyo kusaidia kuokoa maisha.
“Wenzetu Ifakara walianza kufanya utafiti huo kuangalia teknolijia hiyo inavyoweza kuwa muhimu kuhakikisha vitu vinavyohitajika wakati wa dharura vinawafikia walengwa, hasa chanjo za dharura na kinamama wanaojifungua ambao huhitaji damu kwa haraka,” anasema Dk Ulisubisya.
Anasema gharama za teknolojia hiyo ambazo zitalipwa na wadau wa maendeleo, kwa sababu ya unyeti na umuhimu wa teknolojia hiyo kwa kanda ya Afrika Mashariki ni vizuri watengenezaji wasifikirie tu kuzitengenezea Marekani ni vizuri MSD watafute mahali ambako mawazo hayo yatakuwa ya kudumu katika dhana nzima ya kufikia uchumi wa kati.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Zipline , Keller Rinaudo anasema kwa sababu ya uongozi wenye njozi mahiri ya Tanzania waliona ni lazima iwe sehemu ya teknolojia hii katika dunia.
“Mahala pengi dhana ni Waafrika kuchukua yanayotokea nchi za magharibi lakini safari hii mimi na wafanyakazi wangu tunataka nchi za magharibi zije zijifunze huku, tunahitaji ushirikiano wenu na tutaajiri Watanzania katika kulifanikisha hili,” anasema.
Licha ya changamoto ya huduma za dharura upande wa dawa, rufaa pia ni changamoto kwa maeneo yasiyofikika, Msemaji wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Nsachris Mwamaja anasema wizara ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hiyo.
Anasema rufaa za dharura zimekuwa changamoto kwani licha ya kuwepo magari ya wagonjwa, kuna maeneo yana umbali mrefu na miundombinu yake ni changamoto ya kuokoa maisha ya mgonjwa kwa kumpa matibabu kwa wakati.
“Ukisoma kwenye bajeti yetu ya mwaka wa fedha 2017/2018 tumelielezea hilo kwa undani zaidi kwamba tutajenga vituo vya afya vyenye uwezo wa kufanya upasuaji zaidi ya 150, ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuokoa maisha ya mama na mtoto, lakini mipango mingine ya kuokoa maisha ya wagonjwa wa dharura pia inafanywa na wizara,” anasema Mwamaja.
Kuhusu Drones
Mfumo wa kamba wa ndege zisizokuwa na rubani (drones) unaoitwa Zips husafirisha ndege hizo kwa kuziweka kwenye mbawa ndogo za ndege zinazofyatuliwa kutoka kwenye kifaa maalum na kwa kufuata mfumo ulioandaliwa awali kwa kutumia data za eneo.
Faida ya mfumo huo ni kwamba ndege inaweza kukabiliana na hali ya hewa ya upepo mkali kwa muda.
Kwa nadharia, ndege hizo zinaweza kupaa kwa takriban maili 180 ama kilomita 290 kabla ya kuishiwa nguvu za nishati, husafiri chini ya futi 500 kutoka ardhini ama mita 152 kuepuka anga ya juu inayotumiwa na ndege za abiria.
Shirika la Dfid linakadiria kuwa usafirishaji damu na usambazaji wa huduma nyingine za afya kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kutoka nje ya mji mkuu wa Dodoma, kunaweza kuokoa $58,000 kwa mwaka ikilinganishwa na matumizi ya gari ama pikipiki kusambaza huduma hizo.
Namna teknolojia inavyofanya kazi
Kampuni ya Zipline inatumia ndege hizo zisizo na rubani kulepeka mzigo, inaweza kuwa damu salama, dawa au vifaa tiba kwa ajili ya matibabu, ndege hizi kuruka kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 100 kwa saa na pindi zinapofika katika kituo cha afya ama hospitali huangusha mzigo husika kwa parashuti.
Licha ya hivyo kuna aina nyingi za drones zilizozoeleka kama zile za kupigia picha na za kusambazia misaada vitani, lakini ndege zinazotumiwa na Zipline ni za aina ya tofauti kidogo, kampuni hii inatumia Drone ambazo zinamuundo kama ndege ya kawaida ila ni ndogo pia zinakwenda katika mwendokasi mkubwa kushinda drone za matumizi ya kupiga picha.
Mkurugenzi wa Ziplne Rinaudo anasema kampuni hiyo inatengeneza drone ambazo zina mabawa yenye urefu wa futi 6, ndege hiyo ina uwezo wa kukimbia hadi kilomita 110 kwa saa na kwamba zinaweza kubeba uzito wa takribani kilo 1.5 wa dawa ama damu salama na mizigo mingine ambayo ndege hiyo inabeba haizidi uzito huo.
“Zinatumia mfumo wa umeme badala ya mafuta, kila ndege ina betri ambayo inachajiwa kabla ya kuanza safari. Betri ya ndege hii inao uwezo wa kusafiri safari hadi ya kilomita 160 na zaidi kabla ya kuhitaji kuchajiwa tena,” anasema na kuongeza;
“Zinatumia GPS na mitandao ya simu kwa ajili ya kufikia vituo vya afya, pia zina uwezo wa kufanya kazi usiku na mchana, katika mvua, jua na hata upepo mkali. Hurushwa kutoka katika kifaa maalum na husafiri mpaka kituo husika kisha hudondosha mzigo na kurudi kituo cha usambazaji ambako ndege hii hutua katika puto bila uharibifu tayari kwa ajili ya kutumwa tena.”
Dondoo
120 – Ndege zisizokuwa na rubani zitakazotumika kusambaza dawa na vifaa tiba maeneo yasiyofikika Tanzania
15 - Ndege ambazo zinatumika nchini Rwanda kusambaza dawa kwa sasa.
Hata hivyo, anasema lengo la Serikali la kuleta ndege hizo nchini ni kutaka kuongeza upatikanaji wa dawa katika vituo na hospitali zake zote, kwasababu hivi sasa MSD inazisambaza kwa kutumia magari makubwa na madogo.
Na imeingia mkataba na ndege za AirTanzania na usafirishaji kwa njia ya reli unatarajiwa kuanza mwezi ujao.
“Kutumia drones ni njia mojawapo ya kuongeza ufanisi kwa kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura, mahali palipotakiwa kutumia saa mbili mpaka tatu kufikisha dawa, sasa zitafika kwa nusu saa ,” anasema.
Kila jambo linachangamoto
Mkurugenzi huyo wa MSD anasema wagonjwa wengi hukumbana na changamoto pindi waendapo kupata matibabu katika vituo vya afya na hospitali za Serikali.
Anasema wapo ambao huhitaji huduma za dharura lakini huzikosa, kwa mfano wale wanaopata ajali na na kuhitaji kongezewa damu pia wajawazito wanaohitaji tiba ya dharura kama ya kuongezewa damu au upasuaji. Lakini wapo pia wanaong’atwa na nyoka au mbwa.
Akizungumzia uratibu wa usambazaji wa dawa hizo, Bwanakunu anasema Bohari ya Dawa watakuwa na jukumu hilo. Anasema vituo vitakavyotoa taarifa na kuhitaji huduma hiyo ya dharura, vitapokea meseji kwa njia ya simu za kiganjani kutoka MSD ikielezea mzigo uliotumwa. “Vituo vitakuwa vinapokea kwa ujumbe wa simu kupitia simu zao za mkononi na huku itakuwa inadurufu nyaraka. Lakini kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuanza kuzungumza na kitengo cha damu salama kwa kuwa sisi hatusambazi damu,” anasema.
Kiwango cha mzigo kinachosafirishwa na drones
Imeelezwa kuwa ndege hizo ni maalumu kwa ajili ya dharura. Hivyo, hazitakuwa zikisafirisha mzigo mkubwa na zinakwenda kwa haraka na zitakuwa na uwezo wa kufikisha mzigo ndani ya dakika 30. Zitakuwa zikibeba mzigo wenye uzito wa kilogram moja hadi moja na nusu. “Tutakuwa na ndege 30 zitakazokuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 160, ambazo kwa anga ni umbali mrefu katika kila eneo na ndege za kituo kimoja zitakuwa na uwezo wa kufanya safari 2,000 kwa siku,” amefafanua na kuongeza:
“Januari mwakani tutaanza kazi, sisi tunatumia teknolojia hii kuokoa maisha ya binadamu na kupunguza gharama ndiyo hasa lengo letu kwenye mradi huu. Taarifa kuhusu wapi kuna tatizo tutapata kutoka kwenye vituo vya afya, kila kitu kitakuwa kimeunganishwa na mfumo wetu.”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya anasema MSD inatoa huduma kwenye vituo 5,640 nchini, lakini changamoto kubwa ni maeneo yasiyofikika kwa urahisi. Anasema teknolojia hiyo ya ndege zisizo na rubani ambazo kiutaratibu zinatumika vitani Zipline, watatumia teknolojia hiyo kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania. “Wenzetu wa Ifakara walianza kufanya utafiti huo kuangalia teknolijia hiyo inavyoweza kuwa muhimu na kuhakikisha vitu vinavyohitajika wakati wa dharura vinawafikia walengwa, hasa chanjo za dharura na kinamama wanaojifungua ambao huhitaji damu kwa haraka,” anasema Dk Ulisubisya.
Anasema gharama za teknolojia hiyo zitalipwa na wadau wa maendeleo, kwa sababu ya unyeti na umuhimu wa teknolojia hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo, ametoa wito kwa watengenezaji wasifikirie kuzitengenezea Marekani tu, bali ni vema MSD ikatafute mahali ambako mawazo hayo yatakuwa ya kudumu katika dhana nzima ya kufikia uchumi wa kati.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Zipline, Keller Rinaudo anasema kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye miundombinu isiyo rafiki ya usafiri, waliona kuna ulazima nayo iwe sehemu ya kutumia teknolojia hiyo. “Mahala pengi dhana ni Waafrika kuchukua yanayotokea nchi za magharibi, lakini safari hii mimi na wafanyakazi wangu tunataka nchi za magharibi zije zijifunze huku, tunahitaji ushirikiano wenu na tutaajiri Watanzania katika kulifanikisha hili,” anasema. Licha ya changamoto ya huduma za dharura upande wa dawa, rufaa pia ni changamoto kwa maeneo yasiyofikika.
Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Nsachris Mwamaja anasema wizara hiyo inaendelea kupanga mikakati ya kutatua changamoto hiyo.
Anasema licha ya kuwapo kwa magari ya wagonjwa, kuna maeneo yana umbali mrefu na miundombinu yake si rafiki.
“Ukisoma kwenye bajeti yetu ya mwaka wa fedha 2017/2018, tumelielezea hilo kwa undani zaidi kwamba tutajenga vituo vya afya vyenye uwezo wa kufanya upasuaji zaidi ya 150, vitakuwa na uwezo wa kuokoa maisha ya mama na mtoto, lakini mipango mingine ya kuokoa maisha ya wagonjwa wa dharura pia inafanywa na wizara,” anasema Mwamaja.
Kuhusu Drones
Mfumo wa kamba wa ndege zisizokuwa na rubani (drones) unaoitwa Zips husafirisha ndege hizo kwa kuziweka kwenye mbawa ndogo za ndege zinazofyatuliwa kutoka kwenye kifaa maalumu kwa kufuata mfumo ulioandaliwa awali wa kutumia data za eneo.
Faida ya mfumo huo ni kwamba, ndege inaweza kukabiliana na hali ya hewa ya upepo mkali kwa muda.
Kwa nadharia, ndege hizo zinaweza kupaa kwa takriban maili 180 ama kilomita 290 kabla ya kuishiwa nguvu za nishati, husafiri chini ya futi 500 kutoka ardhini ama mita 152 kuepuka anga ya juu inayotumiwa na ndege za abiria.
Shirika la Dfid linakadiria kuwa usafirishaji damu na usambazaji wa huduma nyingine za afya kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kutoka nje ya mji mkuu wa Dodoma, kunaweza kuokoa Dola 58,000 za Marekani kwa mwaka, ikilinganishwa na matumizi ya gari ama pikipiki kusambaza huduma hizo.
Teknolojia inavyofanya kazi
Kampuni ya Zipline inatumia ndege hizo zisizo na rubani kupeleka mzigo, inaweza kuwa damu salama, dawa au vifaa tiba kwa ajili ya matibabu, ndege hizi kuruka kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 100 kwa saa na pindi zinapofika katika kituo cha afya ama hospitali huangusha mzigo husika kwa parachuti na kisha kuondoka.
Licha ya hivyo kuna aina nyingi za drones zilizozoeleka kama zile za kupigia picha na za kusambazia misaada vitani, lakini ndege zinazotumiwa na Zipline ni za aina ya tofauti kidogo, kampuni hii inatumia Drone ambazo zinamuundo kama ndege ya kawaida ila ni ndogo pia zinakwenda katika mwendokasi mkubwa kushinda drone za matumizi ya kupiga picha.
Mkurugenzi wa Ziplne Rinaudo anasema kampuni hiyo inatengeneza drone ambazo zina mabawa yenye urefu wa futi 6, ndege hiyo ina uwezo wa kukimbia hadi kilomita 110 kwa saa na kwamba zinaweza kubeba uzito wa takribani kilo 1.5 wa dawa ama damu salama na mizigo mingine ambayo ndege hiyo inabeba haizidi uzito huo.
ambako ndege hii hutua katika puto bila uharibifu tayari kwa ajili ya kutumwa tena.”
Dondoo
120 – Ndege zisizokuwa na rubani zitakazotumika kusambaza dawa na vifaa tiba maeneo yasiyofikika Tanzania
15 - Ndege ambazo zinatumika nchini Rwanda kusambaza dawa kwa sasa.