Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Christina: Huwa napoteza fahamu maumivu tumbo

Muktasari:

  • Huyu ni Christine Lukasi (40) mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam ambaye amekata tamaa baada ya daktari kumwambia anatakiwa kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye tumbo lake la uzazi ilhali hana fedha za kugharimia matibabu yake.

Kuna wakati hushindwa kuzungumza kutokana na maumivu makali ya tumbo, akipata unafuu, huendelea kuzungumza. Mara nyingi uso wake hauna tabasamu.

Huyu ni Christine Lukasi (40) mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam ambaye amekata tamaa baada ya daktari kumwambia anatakiwa kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye tumbo lake la uzazi ilhali hana fedha za kugharimia matibabu yake.

“Napata maumivu makali. Nimeandikiwa dawa za Sh28,000 kuyatuliza lakini nimeshindwa kununua kwa sababu sina pesa kabisa. Nimekata tamaa,” anasema Christine.

Mwanamke huyo ambaye ni mama ntilie anatakiwa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza na Sh2 milioni zinahitajika kufanikisha upasuaji na gharama nyingine wakati yeye mwenyewe hana chochote na shughuli zake zimesimama akijiuguza.

Barua aliyopewa na ofisi za Serikali za Mtaa wa Magomeni Kondoa anakoishi inaeleza hana uwezo wowote na msaada atakaopewa ndio utakaomsaidia kuokoa uhai wake pale atakapoondolewa uvimbe alionao.

“Anahitaji msaada wa matibabu na kwa barua hii msamaria yeyote anaweza kumsaidia,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Ugonjwa wenyewe

Christina anasema mwaka 2015 alipima na kuambiwa ana uvimbe tumboni na akapewa dawa za kuupunguza. Baada ya kuzitumia maumivu yalipungua lakini Machi yalianza tena.

“Nilienda tena hospitali, hali yangu ikawa mbaya zaidi kwa sababu maumivu nyamekuwa makali, nimepima na daktari ameniambia uvimbe ni mkubwa unatakiwa kuondolewa,” anasema.

Anasema hali yake huwa mbaya zaidi anapokuwa kwenye siku zake na kwamba huwa inamlazimu kutumia kanga nzima kujisitiri kwa sababu pedi za kawaida hazifai kitu.

“Maumivu yakiwa makali huwa napoteza nguvu na wakati mwingine nazimia. Siku moja nilizimia nikipeleka chakula kwa wateja, nilikuja kushtuka baadae nikiwa hospitali,” anasema.

Maumivu makali ya tumbo yalimuanza alipovunja ungo akiwa na miaka 12. Anasema wazazi wake walishangaa kuona mtoto wa umri huo anavunja ungo kwa sababu kwa wakati huo haikuwa kawaida.

“Tangu nikiwa mdogo nilikuwa naumwa sana tumbo, nimetibiwa huku na kule hadi kwa waganga wa kienyeji lakini kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi,” anasema.

Dakari wa Magonjwa ya Wanawake, Chriss Peterson anasema uvimbe katika mfuko wa kizazi hujulikana kama uterine myoma au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

“Kuna wakati uvimbe unaweza kubadilika rangi na kuwa wa njano au kama maji,” anasema.

Kwa kawaida, anasema wanawake wenye kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo huugua zaidi ugonjwa huo ambao baadhi ya dalili zake ni maumivu makali wakati wa hedhi au tendo la ndoa, kuvimba miguu, kuhisi una ujauzito, kupata haja ndogo kwa taabu na kutokwa na uchafu ukeni.

Nyingine ni kupata choo kigumu au kufunga choo, maumivu ya mgongo, miguu kuwaka moto, maumivu ya kichwa na uzazi wa shida.

Msaada: Christine anahitaji msaada wa Sh2 milioni kufanikisha matibabu yake. Kuwasiliana naye mpigie namba 0674 483 530