Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuelewa visababishi vya kisukari aina ya kwanza

Muktasari:

  • Kisukari aina ya kwanza ndiyo aina ya kisukari inayogundulika zaidi kwa watoto. Mtoto anaweza kupata kisukari aina ya kwanza kuanzia akiwa na umri wa miezi sita na kuendelea.

Kisukari aina ya kwanza, kinachojulikana pia kama Type 1 Diabetes, ni ugonjwa sugu unaotokea pale mfumo wa kinga ya mwili, unaposhambulia chembe chembe za kongosho zinazozalisha insulin.

Insulin ni homoni muhimu inayosaidia mwili kutumia sukari kuwa nishati. Bila insulin, sukari hukusanyika kwenye damu na kusababisha kiwango chake kupanda na kuwa hatari.

Kisukari aina ya kwanza ndiyo aina ya kisukari inayogundulika zaidi kwa watoto. Mtoto anaweza kupata kisukari aina ya kwanza kuanzia akiwa na umri wa miezi sita na kuendelea.

Iwapo ugonjwa wa kisukari utagunduliwa kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miezi sita, huo hauitwi kisukari aina ya kwanza, bali huitwa kisukari cha watoto wachanga kwa kitaalum hujulikana ‘ Neonatal Diabetes’.

Sababu kuu ya kisukari aina ya kwanza ni pale kinga ya mwili inapokosea kazi yake ya ulinzi. Badala ya kushambulia vijidudu au virusi vinavyoingia mwilini, inageuka na kushambulia chembe za beta zilizoko kwenye kongosho. Chembe hizi ndizo zinazozalisha insulin. Kadri zinavyoharibiwa, mwili hushindwa kutengeneza insulin ya kutosha, hivyo sukari inabaki damu ikizidi kuongezeka.

Vinasaba ni moja kati ya sababu za aina ya kwanza ya kisukari, utafiti uliowahi kufanywa na National Institutes of Health, ulionyesha kuwa vinasaba vina mchango mkubwa.

Mtu mwenye mzazi, ndugu au jamaa wa karibu aliye na kisukari aina ya kwanza huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo.

Hata hivyo, iwapo mtu wa familia yako ana kisukari aina ya kwanza, kuna uwezekano mdogo zaidi wa wewe au mtoto wako kupata hali hii. Lakini pia, watu wengi walio na kisukari aina ya kwanza hawana mtu yeyote kwenye familia yao mwenye ugonjwa huo.

Maambukizi ya virusi, Baadhi ya virusi kama Coxsackie B, rubella au enterovirus huchochea kinga ya mwili kushambulia kongosho.

Watafiti wanaamini kwamba kwa watu walio na vinasaba fulani, maambukizi ya virusi yanaweza kusababisha kisukari aina ya kwanza miezi au miaka kadhaa baadaye.

Ingawa si sababu ya moja kwa moja, msongo mkubwa wa mawazo au magonjwa sugu, yanaweza kuchochea mashambulizi ya kinga ya mwili kwa watu walio katika hatari.

Kisukari aina ya kwanza hakisababishwi na chakula au kinywaji chochote unachokula au kunywa. Pia, hakuna tiba unayoweza kufanya ili kuzuia ugonjwa huu kujitokeza.

Hata hivyo, kama una kisukari aina ya kwanza, bado ni muhimu kula chakula bora na chenye afya ili kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.

Hakuna tiba ya kuponya kabisa kisukari aina ya kwanza, lakini tafiti zinaendelea duniani kutafuta njia za kuzuia, kutibu, au kurekebisha na kurudisha uwezo wa kongosho kutengeneza insulini.