Haya ndiyo mambo madogo unayoweza kuyafanya na yakakuletea manufaa makubwa kwenye afya yako

Mara nyingi tumekuwa tukidharau mambo madogo madogo sana ambayo yapo ndani ya uwezo wetu kuyatekeleza ambayo kupitia hayo, tungeweza kuzinufaisha afya zetu kwa kiasi kikubwa na kujiepusha na magonjwa hasa yasiyo ya kuambukiza.

Wengi wetu tumejikuta tukipata maradhi mbalimbali na kulazimika kubeba mzigo mkubwa wa matibabu lakini huenda kinga yake ni kufuata tu masharti madogo madogo sana ya kiafya ambayo kwa udogo wake hayalingani na ukubwa wa matibabu unaolazimika kujitwika baada ya homa.

kufanya maamuzi sahihi ya aina ya chakula ili kuepukana na madhara ya kiafya yatokanayo na ulaji wa vyakula ambavyo si salama.

Jumuika na wengine. Jenga tabia ya kuondokana na upweke mara kwa mara na ujumuike na watu wanaokuzunguka.

Kwa kufanya hivi utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuepukana na matatizo ya kisaikolojia kama vile sonona (depression) na hata msongo wa mawazo.

Lakini kwa kufanya hivi itakusaidia kuyamudu matatizo mengine ya kiafya kama vile shinikizo la damu na magonjwa mengine ya kiakili.

Sio lazima uwe na watu wengi sana wa kujumuika nao, hata wachache tu ambao upo karibu nao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwako zaidi ya ujuavyo.

Kujumuika na watu hata kwa saa chache kunaongeza furaha na kisayansi pia imethibitika kunaongeza utendaji kazi wa vichocheo vinavyoleta hisia mwilini na hivyo kukufanya uwe na hari ya kufanya jambo husika.

Hivyo ita marafiki na ujumuike nao kwenye chakula cha jioni na hata sehemu yeyote ya kupumzisha akili angalau mara moja kwa wiki.

Kabili msongo wa mawazo na kila kitu kinachoingilia furaha yako. Moja ya vitu muhimu tunavyowahimiza sana watu ni kujitahidi kuishi maisha yenye afya bora.

Lakini ukweli ni kwamba hamna maisha yenye afya bora pasipokuwa na furaha.

Naomba ieleweke kuwa, kukosa furaha kunaweza kusababisha matatizo mengi na makubwa ya kiafya zaidi ya vile unavyoweza kufikiria.

Hata sisi wahudumu wa afya huwa tunakutana na changamoto kubwa kuwatibu wagonjwa wenye matatizo ya kisaikolojia na hasa waliokosa furaha kuliko wagonjwa wa aina nyingine yeyote ile.

Kila mmoja amewahi kupitia hali hii, lakini msongo wa mawazo ukizidi unaweza kusababisha kukaza kwa mishipa ya damu na kuongezeka kwa kasi ya mapigo ya moyo, ambayo yakidumu sasa husababisha matatizo kama vile magonjwa ya moyo.