Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufanye nini ndoa yako ikivunjika?

Baadhi ya ndoa huvunjika haraka ilhali nyingine huonekana kuchukua muda mrefu. Haijalishi kisababishi ni nini, ndoa ikivunjika unaweza kuelemewa na hisia mbalimbali. Hisia kama vile, huzuni, hasira, maumivu, kuhofu kuhusu wakati wako ujao, upweke, kuchanganyikiwa kutokana na maamuzi unayopaswa kufanya na hisia ya kushindwa kwa sababu ya ndoto na mipango iliyoharibika.

Ni muhimu kuchagua njia ambayo utatumia kushughulikia hali ya kutengana, kwa kuwa itakuwa na matokeo katika maisha yako yanayobakia.

Ikiwa hutashughulikia maumivu yako, na utajiiruhusu uwe na uchungu kwa muda mrefu, utakosa furaha katika maisha yako kwa muda mrefu. Acha uchungu na hasira ziondoke. Ona kutengana kuwa fursa ya kujichunguza na kujua uwezo wako, rasilimali zako na ndoto zako, na ufanye mabadiliko mapya kamili na yenye faida kwa maisha yako ikihitajika.

Ikiwa wewe ama mtu mwingine unayemjua anapitia hali ya kutengana au talaka, tunatumaini kwamba makala hii itakusaidia kuelewa na kukabiliana na changamoto katika kipindi hiki cha mabadiliko.
 

Mambo unayoweza kufanya

Watu wengi ambao wamepitia hali ya kutengana na kutalikiana wanahisi uchungu kama unaopitia wewe kwa sasa na wengi hatimaye wamebadilika na kuwa imara kuliko ilivyokuwa zamani.
Hata hivyo, unapoendelea kukabiliana na hali hii mpya maishani, unahitaji ustadi na msaada wa kihisia. Hapa chini kuna orodha ya mambo unayoweza kufanya:
 

Zungumza na mtu unayemtumaini

Kuzungumza na mshiriki wa familia ama rafiki kunaweza kukusaidia kuondokana na hali ya kuchanganyikiwa na hasira. Uwe mwangalifu usiwatwishe watoto wako mzigo huu wa hisia.

Hakikisha kwamba mtu unayemshirikisha siri zako ni yule mwenye kutumainika ili uweze kuwa huru kumweleza hisia zako za ndani kabisa. Unaweza kumtafuta mtu ambaye amepitia hali ya kutengana ama kutalikiana, mtu wa aina hii anaweza kutoa msaada unaofaa.


Dumisha ratiba nzuri kwa ajili yako na watoto wako

Ni muhimu kuwa na hisia ya uimara katika kipindi hicho cha mabadiliko makubwa na yenye maumivu. Hili ni muhimu sana kwa ajili ya watoto wako: kadiri ulimwengu unapoendelea katika hali yake, ndivyo ambavyo itawasaidia kukabiliana mabadiliko ambayo watahitaji kufanya.
 

Dumisha mawasiliano ya wazi na watoto wako

Watoto wanahitaji kujua kwamba hawajapoteza upendo na msaada kutoka kwa wazazi wao, na kwamba wao si kisababishi cha kutengana au talaka ya wazazi. Zungumza nao kwa uwazi kuhusu mipango ya mabadiliko katika maisha yao mapya.
 

Tunza afya yako

Unaweza kujikuta umesahau kula kulingana na ratiba kwa sababu umekuwa na wasiwasi kwa muda mwingi. Hili litafanya upoteze nguvu ama kushambuliwa na magonjwa katika kipindi ambacho unapaswa kuwa na afya na nguvu. Tunza afya yako kwa kula chakula kwa ukawaida na kulala vya kutosha. Pia, unapaswa kuwa na ratiba ya kufanya mazoezi kwa ukawaida.
 

Jifunze mbinu za kukabiliana na msongo wa mawazo

Kuna vitabu vingi ambavyo unaweza kusoma ili kujua jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo, na unaweza kupata taarifa nyingi za kitaalamu za kukusaidia. Vitafute vitabu hivyo katika maktaba iliyo karibu nawe au hata mitandaoni.

Yapo pia masomo mengi kwenye chaneli za youtube, masomo yenye lugha mbalimbali kadiri unavyozielewa. Unaweza kutembelea na kujiunga “subscribe” kwenye chaneli ya “Chris Mauki” na kujifunza namna bora za kukabiliana na msongo wa mawazo.

Kabiliana na hali ya kutengana, matatizo unayotarajia na hisia kwa kujiuliza mwenyewe, "Ninapaswa kufanya nini leo?" Jaribu kupunguza hofu kuhusu vitu ambavyo huwezi kufanya chochote kuvihusu kama vile mambo ya juma lijalo ama mwezi ujao.

Wakati utakapofika shughulikia kama ulivyofanya kwa yale mengine yaliyopita – ishi kwa siku moja pekee.
Epuka kufanya maamuzi makubwa hadi maisha yako yatakapotengamaa.

Baadhi ya maamuzi yanapaswa kufanywa haraka, maamuzi hayo ni kama kupanga nyumba na kufanya mipango ya shule kwa ajili ya watoto wako, kama ulikuwa huna ajira, tafuta ajira. Hata hivyo, unaweza kuweka kando maamuzi mengine hadi pale “vumbi litakapokuwa limetulia." Itakuwa bora ukijipa muda kabla ya kufanya maamuzi ya kubadilisha ajira, kuhama, kurudi shule ama kuanzisha mahusiano mapya.
 

Ruhusu muda upite ili upone

Familia yako na rafiki zako wanaweza kukutia moyo "uchangamke" na "kuendelea na maisha" hata kabla hujawa tayari. Kwa kawaida, hilo hutokea kwa kuwa watu wanaokujali wanajisikia vibaya kukuona huna furaha.

Ingawa hangaiko lao linaeleweka, unahitaji kujipatia muda wa kutosha ili kupona. Kupoteza ndoa haijalishi kulikuwa na ugumu kiasi gani, husababisha makovu, na yanahitaji muda ili kupona. Tenga muda mtulivu wa kuwa peke yako ili kutafakari, kulia, ama tu muda wa wewe kuwa peke yako.
 

Tafuta msaada wa kitaalamu unapohitaji

Utakabili matatizo ya kisheria na kihisia unapopata talaka ama kutengana, na huenda ukahitaji msaada wa kitaalamu. Kwa msaada wa kisheria, tafuta msaada kutoka kwa mwanasheria.
Ikiwa unakabili msongo wa mawazo mkali, mtaalamu wa ushauri. Pia, inaweza kukusaidia ikiwa utaongea na viongozi wa dini yako.