Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utoke vipi ‘holidays’ za mwisho wa mwaka

Mwisho wa mwaka pamoja na kuongozana na sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya, familia nyingi huwa katika mapumziko.

Kutokana na pilikapilika za watoto shule na kufanya kazi kwa mwaka mzima, baadhi ya familia huamua kusafiri kwa ajili ya kwenda mapumziko (holidays) kwa maana ya kuachana na yale waliyokuwa wakipambana nayo na kuamua kusherehekea kwa pamoja na ndugu, jamaa, marafiki au familia pekee.

Hata hivyo, ili mapumzo yaende vizuri kama umeamua kwenda nje ya nchi, mkoani au kukaa hotelini kwa muda fulani kulingana na matakwa ya mtu, uchaguzi wa mavazi ni kitu cha muhimu.

Inawezekana unazo nguo za aina nyingi na nyingine na haujazinunua bado lakini cha kujiuliza ni mavazi ya aina gani utakayoyavaa pindi ukiwa mapumziko na marafiki zako, mke, mumeo, ndugu au watoto.

Kwa hiyo kulingana na jinsia yako unapaswa kuchangua nguo zitakazokuweka bomba na huru muda wote iwe katika matembezi ya hapa na pale, mbuga za wanyama, eneo la hotelini au ufukwe.

Katika kipindi hiki kuna mitindo ya mavazi yatakayokufanya upendeze na kukupa uhuru ukiwa sehemu za mapumziko.

Kwa mujibu wa wanamitindo ya mavazi, epuka kuvaa mavazi rasmi kwa sababu ni kipindi ambacho mwili na akili yako inataka kuwa huru.
Sio kipindi cha kuvaa suti na nguo ambazo zimekunyima uhuru katika mfumo rasmi wa kutafuta riziki.
 

Fulana nyepesi

Kwa upande wa wanaume, hizi ni nguo ambazo hutakiwi kukosa wakati wa mapumziko kwa sabubu zitakupa mvuto wa kipekee na uhuru wakati wote unapokuwa sehemu za kustarehe hasa ukivalia na kaptula huku viatu ‘ukapigilia’ sendo.

Mwanamitindo Mwamvi Daniel anasema fulana nyepesi zina mvuto ambao humfanya mvaaji kupendeza na kupata hewa.
Lakini wanawake hawatakuwa mbali na fasheni hii endapo watalipangilia vyema vazi hili.
 

Nguo za kuzungusha ‘wrap dresses’

Hizi ni nguo ambazo hupendelewa kuvaliwa na wanawake kwa sababu huwafanya wanaovaa kuwa huru. Unapokuwa mapumziko vaa nguo hizi hasa zilizoshonwa kwa kitambaa chepesi kinachowezesha hewa kupita na mwili kuwa huru. Nguo hizi zinaweza kuwa ni sketi au gauni; kwa upande wa sketi vaa na ‘crop top’ au blauzi ya mikono membamba.

Pia, kama upo sehemu za fukwe unaweza kuvaa sketi za kuzungusha za kitambaa cha Bahama kwa sababu kina pamba laini.
Veronica Mambwe anasema nguo za kuzungusha humfanya ajihisi huru na humpa urahisi kuivaa hata akiongezeka mwili.
Anasema kwa kipindi hiki ambacho yupo mapumziko anaona ndio wakati wake wa kuwa huru.
 

Bwanga

Vazi hili hunoga likiwa limeshonwa kwa kitambaa chepesi.
Nguo hizi hazichagui umbile la wanene na wembamba wote wanavaa kwa staili mbalimbali.

Mmoja wa wabunifu wa mavazi anayejukana kwa jina la Frivola anasema bwanga ni nguo huru kwa maumbile yote ya wanawake hasa ukilipatia kitambaa chenye maua mazuri na yenye rangi inayovutia.

Hili vazi sio la kulikosa kipindi hiki kwa sababu huuachia mwili na wakati wowote ule linapovaliwa mvaaji huwa huru.

Vazi hili huvaliwa sehemu yoyote na unaweza kuvalia na topu kulingana na rangi za bwanga utakalolivaa.

Veronica Mambwe anasema nguo za kuzungusha humfanya ajihisi huru na humpa urahisi kuivaa hata akiongezeka mwili. Anasema kwa kipindi hiki ambacho yupo mapumziko anaona ndio wakati wake wa kuwa huru.
 

Kimono

Hili ni vazi ambalo huvaliwa juu ya nguo, muundo wake umetengenezwa kwa uwazi wa mbele na kuipa nafasi nguo iliyovaliwa ndani kuonekana vizuri. Katika mapumziko baadhi ya watu hupendelea kwenda sehemu za fukwe; huhitaji kujikinga na upepo, hivyo kimono ni vazi sahihi kwa sababu huwapa wanawake mwonekano wa kipekee.

Mwajuma Selemani anasema licha ya kipindi cha mapumziko lakini kujistiri kwa mwanamke kupo palepale.

“Mimi nikitinga kimono changu ndani nikavaa na taiti ndefu juu vesti imeisha hiyo(vazi lake limekamilika,” anasema Mwajuma.
 

Nguo za kufanana ‘two pieces’

Hizi ni aina ya nguo ambazo zimeushika ulimwengu wa mitindo mwaka huu japokuwa awali zilishawahi kuvaliwa.

Baada ya kutambulishwa na kuvaliwa na watu wengi zimeendelea kubamba, hivyo katika kipindi cha mapumziko usiache hii fasheni ikupite.

Jackson Jorwa anasema akiwa mapumziko hupendelea kuvaa kaptula na shati la mikono mifupi vinavyofanana.

Zulfa Hussein anasema akivaa suruali na shati ambazo zimeshonwa kwa vitambaa vya kufanana hujiona amependeza na huwa huru.
Vazi hili huvaliwa na jinsia zote, kwa upande wa wanaume huwa ni shati na kaptula na wakati mwingine suruali japo kwa kipindi cha mapumziko kaptula ndio hufaa zaidi.
 

Sendo na kandambili ‘slippers’

Sio kipindi cha kuvaa viatu na soksi kama unaenda ofisini au shughuli rasmi unatakiwa uvae viatu vitakavyo kupatia hewa na kukuacha huru bila kuathiri muonekano wako wa kuvutia.Tydo Master, mbunifu wa mavazi na mwanamitindo, anasema sendo na kandambili zinavutia zaidi unapokuwa upo sehemu za fukwe kwa sababu ya kutoupa nafasi mchanga kukaa kutokana na uwazi uliopo.
Ni vyema kuvaa sendo au kandambili kipindi hiki cha mapumziko kuendana na aina ya nguo utakazovaa.
 

Vinjunga (kaptula)

Ni kipindi cha kujiachia na kupendeza zaidi, sio wakati wa kujibanabana kutokelezea na kinjunga katika mtoko wako wa mapumziko. Kwa wanawake unaweza kuvaa kinjunga kinachoachia mwili au wakati mwingine kubana kwa juu na kuvalia na topu au shati huku ukiwa umevaa viatu aina ya sendo.

Pia, wanaume wanaweza kuvaa vinjunga na shati au vesti.
Akizungumza na Mwananchi Mkaile Jamal anasema kinjunga ni vazi linalowapa uhuru wavaaji hasa kutokana na joto kuongezeka kwa kiwango cha juu, hivyo huwafanya wawe huru na kupata hewa.