Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIPODOZI NA MAPAMBO : Je, Wanaume wanapenda wanawake wanaojiremba kupita kiasi?

Muktasari:

  • Kubandika kucha, kope, lenzi za macho na kuchora wanja wa tattoo. Pia, kubandika nywele bandia kwa kutumia gundi, kupaka mkorogo, kutoboa ulimi, kitovu na urembo mwingine wa kisasa.

Kuna aina nyingi za urembo zinazovutia, zinazokera, zinazopendeza na kuchukiza zote zinatumiwa na wanawake na ikionekana wanaofanya hivyo ndiyo wa mjini na kisasa.

Kubandika kucha, kope, lenzi za macho na kuchora wanja wa tattoo. Pia, kubandika nywele bandia kwa kutumia gundi, kupaka mkorogo, kutoboa ulimi, kitovu na urembo mwingine wa kisasa.

Kuna dhana imejengeka kwa baadhi ya watu kuwa wanawake wanajiremba kwa ajili ya wanaume. Hakuna utafiti uliothibitisha hilo lakini uhalisia unaonyesha kutokana na ukweli kuwa mwanamke anapojiandaa kwenda kuonana na mwanaume, mpenzi wake au watu wa Pwani wanavyowaita ‘mtu wangu’, hujiremba na kujinakshi kwa uturi na mapambo ya kila aina.

Swali ni je, wanaume wanapenda wanawake wanaojiremba kupita kiasi, au wanawake wanafikiri wanaume wanapenda wao wajirembe?

Kidunda Mwita anasema anapenda kutizama wanawake waliojiremba kwa sababu ni kitu kipya machoni mwake lakini hatamani kuwa na mwanamke wa aina hiyo.

Anasema kitu kinachomkera ni mwanamke kuwa na kucha ndefu za bandia huku akiwa amejitwisha mzigo wa nywele kichwani.

“Tena bora awe na fedha atatengeneza kwa wanaojua angalau ukiziona unaweza kujidanganya ni zake, akitengenezwa Uswahilini anakuwa kama amepona wazimu hivi karibuni kwa kweli sipendi,” anasema.

Halima Yahaya anasema hajawahi kuwa na kucha zake tangu alipoanza kubandika miaka mitatu iliyopita na hajawahi kupata madhara na hufanya hivyo ili awe na mikono miguu inayovutia.

“Kucha zangu mbaya, hazivutii hata nikiwa mezani nagonga mvinyo nikiinua bilauli naona watu wote wananiangalia kwa jicho baya, lakini bebi wangu anapenda na huwa ananipa fedha za kufanya hivyo,” anasema Halima.

Beatrice Christian anasema mumewe anapenda kumuona akiwa nadhifu ndiyo maana hujiremba.

“Anapenda nisuke rasta na siwezi kufanya hivyo kila siku ndiyo maana siku nyingine nabandika nywele, kucha, kope na ninavutia zaidi nikifanya hivyo, ”anasema.

Tina Jazalo anasema anafahamu kuwa zina madhara lakini hawezi kuacha kwa sababu anapenda kufanya hivyo na akijiremba anakuwa jasiri , anayejiamini kupita mbele za watu.

Kama sijabandika kope, kucha, nywele ndefu najiona natisha na siwezi kupita mbele za watu hasa wanaume, lakini nikifanya hivyo ninaweza kuhutubia hata mkutano wakiwa wao pekee, kwa sababu najiamini na ninaamini navutia na kuwavutia wao pia,” anasema Jazalo.

Wanaume watoa ya moyoni

Seveline Lawrence

Kujiremba kupita kiasi siyo utamaduni wa Mwafrika na ndiyo maana wengi wa wanaofanya hivyo wanaishia kuwa nyumba ndogo.

Wanatumia fedha nyingi kumuwinda mwanaume ambaye mwishowe atamkimbia badala ya kuzitumia kwa maendeleo.

Siwapendi na hata nikiwaona najisikia vibaya. Wengine vipodozi vinawakataa wanakuwa kama wameungua. Siwezi kumpenda mwanamke wa aina hiyo kwa sababu siwezi kwenda naye hata mbele ya jamaa zangu.

Deus Gwanchele

Sitaki hata kuwaona kwa sababu ninamfahamu mwanamke mwenye viashiria vya saratani kwenye kucha, iliyotokana na kubandika kwa kutumia gundi.

Niliwahi kumshauri aache kubandika kucha lakini unajua mambo ya wanawake tena, hakunisikiliza.

Ninafahamu madhara ya kope na mkorogo ndiyo maana siwapendi, nilijaribu bila mafanikio kukomesha tabia hiyo kwa mwanamke wangu ilishindikana, lakini siyo jambo jema kabisa natamani wanawake wote wafahamu hilo.

Lamson John

Nashangaa wanawake wanajiremba kwa ajili ya nani kwa sababu sidhani kama wanaume wengi wanapenda wanawake wenye mwili nusu wao, nusu bandia.

Yaani unakuwa na mwanamke na ukimwangalia kila kitu cha bandia hadi ngozi, hata kama ana tabia nzuri lakini huna uhuru wa kumpeleka kwa rafiki zao wala ndugu zako kwa sababu hawatakuelewa.

Ukweli ni kwamba wanaume hatupendi wanawake wajipodoe kupita kiasi. Uasili ndiyo unaomfanya mwanamke avutie.

Salim Jumaa

Huwa najiuliza maswali hivi hawa wanawake wanajiremba kwa sababu gani? Wanamridhisha nani?

Kama wanafanya hivyo kujifurahisha wenyewe hakuna neno, lakini kama kuna mtu wanamlenga na ni wanaume, basi watakuwa wanakosea. wanaume tunapenda mwanamke ajirembe kiasi, siyo ajikwatue mpaka umsahau. Siku hizi wanawake wengi wana macho mekundu kwa ajili ya kubandika vitu machoni, hata ukimuona mwanamke mweupe unajiuliza ngozi yake bandia, kwa kweli wanakera na wanajitafutia maradhi.