Aubameyang kufuata mapesa Man United

Endapo nahodha wa Arsenal, Pierre- Emerick Aubameyang atajiunga na Manchester United si kwasababu ya tamaa.

Man United inamtolea macho mshambuliaji huyo ikitaka kumsajili katika majira ya kiangazi msimu ujao.

Baada ya kucheza kwa kiwango bora, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Gabon, hataongoza mkataba na Arsenal. Kinara huyo wa mabao ana thamani ya Pauni50 milioni.

Klabu nyingine inayomtaka Ulaya mshambuliaji huyo ni Barcelona ambayo inataka huduma yake baada ya kuvutiwa na kiwango chake.

Akiwa amefunga mabao 17 akishika nafasi ya pili nyuma ya Jamie Vardy aliyefunga 19, Aubameyang amejiweka sokoni kutokana na ubora wake.

Wakati usajili wa nyota huyo ukiibua mjadala, nguli wa zamani wa Arsenal Paul Merson amesema ni fedha pekee ndio itampeleka Man United.

Merson alisema Aubameng anataka fedha kwa kuwa ana umri wa miaka 30 ambao unamfanya asake maisha mapya kabla ya kustaafu.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema hana hakika kama Aubameyang ataongeza mkataba kwa kuwa tayari ameonyesha nia ya kuondoka Emirates.

Arsenal italazimika kuuza mchezaji nyota ili ipate fedha za kununua wachezaji hodari katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

“Sidhani kama Aubameyang anataka kujiunga na Manchester United kwa tamaa. Bila shaka atafuata pesa kwasababu ya umri,”alisema nguli huyo.

Nguli huyo alisema pia mchezaji huyo hawezi kutua Man United kwenda kuisaidia kutwaa ubingwa kwa kuwa hana hakika na jambo hilo.