Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI: Nywila nyingi kwenye simu zina madhara

Muktasari:

Ipo mifumo tofauti ya nywila kulingana na mahitaji ya mtumiaji. Wapo wanaotumia tarakimu, maneno, alama za mwili au mchanganyiko wa viwili au zaidi ya vilivyoorodheshwa.

Vifaa vingi vinavyotumia mfumo wa kielektroniki vinahitaji nywila ( password), kwa ajili ya usalama wa taarifa zilizomo. Simu, kompyuta, milango, kadi za benki au sanduku la kuhifadhia vitu vya thamani ni baadhi ya vifaa hivyo.

Ipo mifumo tofauti ya nywila kulingana na mahitaji ya mtumiaji. Wapo wanaotumia tarakimu, maneno, alama za mwili au mchanganyiko wa viwili au zaidi ya vilivyoorodheshwa.

Imekuwa desturi kwa watumiaji wengi wa simu za kisasa za mkononi (smartphone) kuweka nywila kwa ajili ya ulinzi ili kuepuka kukaguliwa au ufahari. Matumizi haya yamevuka mipaka pamoja kiasi cha kuwa vigumu mhusika kupata msaada anapopatwa na tatizo.

Wapo walioweka nywila kuanzia simu inapowashwa, kwenye kitabu cha majina, file la picha, ujumbe mfupi, kumbukumbu za mawasiliano yaliyofanywa, intaneti hata programu za WhatsApp, Twitter na Telegram.

Kwa kutambua matatizo huja bila kugonga hodi, mmiliki wa kifaa cha kielektroniki anaweza akakumbwa na lolote ambalo litahitaji mtu mwingine kutumia kifaa chake na hapo ndipo shughuli inapoanzia.

Simu yenye nywila nyingi kiasi hicho hukatisha tamaa ya anayetaka kutoa msaada kufanikisha adhma hiyo. Chukulia mwenye simu hiyo amepata ajali au ugonjwa wa ghafla na walio karibu wanataka kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa zake kwa kutumia simu yake. Patakuwa na shughuli nzito.

Kwa haraka haraka kuna matatizo kama matatu yanayoweza kujitokeza endapo nywila zitazidi ukomo kwenye simu ya mtumiaji ambaye asingeziweka msaada wa haraka ungepatikana.

Ikitokea umepata ajali yoyote mbali na ndugu au jamaa zako msaada wa kwanza utapata kwa watu wa karibu ambao watahitaji kutoa taarifa ila endapo simu ina nywila kila sehemu ni wazi hutoweza kupata msaada zaidi.

Pili, ajali itakayosababisha kifo watoa huduma watahitaji kutumia simu yako kufikisha taarifa kwa familia yako au mtu yeyote aliyemo kwenye simu, sasa kama nywila zitakuwa nyingi kupitiliza ni dhahiri hakuna msaada watakaoweza kuutoa ili kuushughulikia mwili ipasavyo.

Tatu ni unapopoteza simu endapo itaokotwa na msamaria mwema ambaye angependa airudishe kwako, hatoweza kufanya hivyo kwani atashindwa kuwasiliana na watu wako wa karibu kwa kutozifahamu nywila ulizoweka kila mahali.

Sipingi kuweka nywila ila ziwekwe maeneo muhimu ambayo hayatazuia kusaidiwa pindi ikihitajika. Nywila zikiwa nyingi, siyo kwenye simu pekee, ni rahisi kupoteza kumbukumbu itakapotokea umesahau. Simu inaweza kujifunga ukikosea mara kadhaa.

Simu ambayo imewekwa nywila zisizowiana na kujifunga inatakiwa kufutwa kumbukumbu zote hivyo kusababisha usumbufu wa kupata mawasiliano ya watu muhimu ulikuwa nao.

Naunga mkono uwekaji wa nywila faili la picha au gallery kwani watu wengi wakipewa simu ya mtu hukimbilia huko ili waangalie picha na video. Hata picha wasizotakiwa kuziona huwa bayana kwao.

Hilo ni faili ambalo linatakiwa kuwekewa nywila mengine ni programu za mitandao ya kijamii kwa sababu ni muhimu kulinda taarifa na mawasiliano yako binafsi lakini siyo kiasi cha kushindwa kupata msaada.

Licha ya maboresho yaliyomo kwenye simu za kisasa yasitufanye kuweka nywila kila sehemu.