Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walianza na vipara, sasa ngozi ya Albino

Muktasari:

  • Binadamu ana mambo ya ajabu sana. Hataki kukubali kwamba ana udhaifu mkubwa wa kutoshughulisha kichwa chake, lakini anataka kuonekana kwamba ndiye kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wengine wote. Anapotaka kula kuku kirahisi anamnenepesha kwa vidonge vya ARV ambavyo vitamdhuru yeye mwenyewe haraka sana.

Kuna habari imeshika mitandaoni kwamba Kanisa moja la Mexico linauza viwanja mbinguni. Tangazo lao linasema wanauza viwanja mbingini kwa dola 100 za kimarekani (takribani T250,000) kwa Mita za Mraba. Mchungaji wao amesema ameongea na Mungu na ameruhusiwa kuuza ploti za mbinguni. Hadi sasa haijajulikana ni watu wangapi wanaodai kuwa na akili timamu walionasa.

Binadamu ana mambo ya ajabu sana. Hataki kukubali kwamba ana udhaifu mkubwa wa kutoshughulisha kichwa chake, lakini anataka kuonekana kwamba ndiye kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wengine wote. Anapotaka kula kuku kirahisi anamnenepesha kwa vidonge vya ARV ambavyo vitamdhuru yeye mwenyewe haraka sana.

 Wakati panya anapomkuta kuku huyo mezani wala hashughuliki naye. Akikuta dagaa ndiyo atahangaika.

Binadamu anayakoboa mahindi kwa kutoa kiini chenye lishe yenye faida kwake, kisha anasaga sehemu iliyobaki na kupata kitu kinachofanana na chokaa. Kwa bahati mbaya anakosa uwiano ulioumbwa kwenye mahindi na mwishowe anaambulia maradhi yanayosababishwa na wanga uliopitiliza.

 Mwenzake panya anapoingia kwenye kapu la mahindi anashughulika na viini tu, akimwachia binadamu pumba na chokaa.

Kwa kudhani hashindwi na mdudu wala mnyama yeyote, binadamu alianzisha vita vya kimaslahi dhidi ya panya. Akamtengenezea silaha za maangamizi ambazo kama panya wasingelikuwa werevu wangeangamia wote. Ingawaje wengi walikufa, lakini bado hatuwawezi kwani wao hula mlo kamili na wanatumia vichwa vyao kwa usahihi.

Pamoja na kunaswa na mitego ya chuma, madema, gundi na kuuawa kwa sumu, lakini panya anaonekana kuishinda vita. Hadi binadamu akaamua kuwakamata na kuwaingiza maabara wakiwa hai. Kila alipogundua sumu ya kuua binadamu wenzake au dawa ya kutibu maradhi, majaribio yake yalianzia kwa panya.

Lakini kwa hali jinsi ilivyo, wanadamu wanaweza kujiangamiza wote wakawaacha panya. Ebu fikiria akili zetu jinsi zinavyotofautiana na hali halisi tunapigana wenyewe kwa wenyewe kunyang’anyana rasilimali tulizotunukiwa, tunafanya ramli chonganishi na kudhulumu uhai wa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, na tunaharibu mazingira kwa makusudi pamoja na kujinyima maji salama na hewa safi.

Kipindi cha nyuma ramli chonganishi ziliwaangamiza watu wenye ualaza na vipara vya asili. Jamii ya wavuvi ilidanganywa kwamba ati vichwa hivyo vina mvuto kwa samaki, hivyo wenye vipara wakalazimika kujificha au kuhama kabisa huku waking’ang’aniza kofia vichwani mwao.

Baadaye ramli zikawasakama wazee wenye macho mekundu. Balaa kubwa lilizuka huko kanda ya ziwa katika miaka ya themanini. Kama vile haitoshi, wachafuzi wakuu wa hali ya hewa wakaiona fursa ya binadamu kutaka maisha salama. Wakatangaza kwamba huko kwenye sayari ya Mars kuna maji salama na hewa safi, hivyo ukiwapa fedha wanakutayarishia makazi sayarini huko! Baada ya hiyo ndiyo inakuja hii ya Kanisa la Mexico kupata udalali wa kuuza viwanja vya mbinguni.

Amini usiamini tayari kuna umati umeshapeleka maokoto Kanisani hapo. Mimi siangalii pale tulipoangukia, bali pale tulipojikwaa ili kama kuna jiwe ama kisiki basi tuking’oe na tusijikwae tena. Haya maisha ya kutotumia vichwa vyetu na kutegemea kulishwa kila jambo itatumaliza. Mbwa wako anapojisikia vibaya huenda kutafuna aina fulani za majani na anapata ahueni. Sasa kwa nini wewe ukiambiwa “dawa yako si dawa, kunywa hii” ukurupuke kuifakamia?

Sisi tuliharibiwa vichwa kwa kuambiwa kwamba tu masikini na hatuwezi lolote. Kama ni kweli, wao walifuata nini kwenye Chuo cha Timbuktu nchini Mali na kwenye mapiramidi ya Misri? Wanatafuta nini kwenye chakula na dawa zetu? Isijekuwa ni yale aliyosema Mwalimu kwamba wanakwambia “hiyo siyo dhahabu, dhahabu ni hii” halafu mkabadilishana kwa yeye kuchukua dhahabu nawe akakuachia kipande cha chupa.

Msione barabara zao zikifurika magari na miji yao iking’ara kuwa ni maendeleo. Lazima mtumie akili kujua matatizo yanayowakabili katika maendeleo yao. Kama hamjawahi kusikia, waliwahi kuufunika mji mzima kwa kioo na ndani ya mji wakamwaga uturi na taa za rangi. Ziko wapi hivi sasa ngebe zile?

Hao ndiyo waliotupeleka kwenye uzazi wa kubania watoto na sasa tunajuta. Dunia nzima sasa inaona umuhimu wa rasilimali watu. Wengine wamefikia hata kuwalipa wageni waende kuzaliana huko kwao tena kwa malipo. Bila shaka walijua tukiwa wengi tutatoboa. Tunakumbuka shuka wakati kumeshakucha.

Haohao wakatushawishi tuache mbegu za asili na kutumia mbegu chotara. Cha ajabu wao walitumia mbegu chotara kwa ajili ya kutuuzia sisi mazao yake. Tulipokuja kushtuka kwamba tunapigwa tulikuwa tushapigika kweli. Ndiyo mambo ya kubadilishana dhahabu OG na vipande vya chupa. Bora tungejua mapema tungefanya biashara ya vipande vya chupa kwa dhahabu feki iwe ngoma droo.

Hivi sasa kuna swaga za “singo maza” na “singo faza”. Humu hamna ukweli hata kidogo kwani hakuna usingo kwa madoni watano: Kuna wa chakula, wa kodi ya nyumba, wa ada za watoto, wa manunuzi na matengenezo ya gari na wa kuondoa stress. Ni uwongo usio na tija, tena mnawafundisha watoto kudanga wangali wadogo.