Burham awasili London kuapishwa ubunge, atajwa kurithi mikoba ya Waziri Mkuu
Andy Burnham akiwasili jijini London akitokea Manchester kwa ajili ya kuapishwa rasmi bungeni Westminster kuwa Mbunge wa Makerfield. Picha na Mtandao
Andy Burnham, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, amewasili jijini London kwa treni akitokea Manchester kwa ajili ya kuapishwa rasmi bungeni Westminster kuwa Mbunge wa Makerfield.
Kuapishwa kwake kuwa mbunge kunafungua njia ya yeye kuchukua mikoba ya uongozi na kuwania nafasi ya Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
Kuwasili kwa mwanasiasa huyo mahiri, ambaye hadi wiki iliyopita alikuwa Meya wa Greater Manchester, kunajiri saa chache baada ya Keir Starmer kutangaza kujiuzulu rasmi wadhifa wa Waziri Mkuu kutokana na shinikizo kubwa la kisiasa ndani ya Chama cha Labour.
Andy Burnham akiwasili jijini London akitokea Manchester kwa ajili ya kuapishwa rasmi bungeni Westminster kuwa Mbunge wa Makerfield. Picha na Mtandao
Njia ya Burnham kuwa Waziri Mkuu
Moja ya matukio makubwa yaliyosafisha njia ya Burnham kuelekea kuwa Waziri Mkuu ni uamuzi wa mpinzani wake mkuu wa zamani na aliyekuwa Katibu wa Afya Kivuli, Wes Streeting, kujiondoa katika mbio za kuwania uongozi wa chama.
Streeting alitangaza hadharani kumuunga mkono Burnham, akieleza kuwa nchi kwa sasa inahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kuunganisha chama na kurudisha imani ya wapiga kura kwa haraka.
Kujiondoa kwa Streeting kunamaanisha kuwa Burnham hana mpinzani mwenye nguvu aliyesalia, jambo linalomfanya kuwa mgombea pekee wa maridhiano ambaye atatangazwa kuwa kiongozi mpya bila kupingwa.
Hatua zilizobaki kabla ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu
Licha ya kuwasili London na kupewa nafasi hiyo, itifaki za kisheria za Uingereza lazima zifuatwe kabla ya kukabidhiwa rasmi funguo za Ofisi ya Namba 10 Downing Street.
Andy Burnham anatarajiwa kuapishwa rasmi bungeni Westminster kuwa Mbunge wa Makerfield. Picha na Mtandao
Kuapishwa ubunge
Hatua ya kwanza kabisa kwa Burnham ni kuapishwa bungeni kama Mbunge wa Makerfield ili kupata uhalali wa kisheria wa kuingia bungeni, na tayari ameapishwa.
Uteuzi ndani ya chama Chama cha Labour kitafungua rasmi mchakato wa uteuzi wa dharura wa kiongozi mpya.
Kupita bila kupingwa
Kwa kuwa mawaziri na wabunge wengi wameweka msimamo wa kumuunga mkono yeye pekee, jina lake litapitishwa bila kuhitaji kura za kitaifa za wanachama.
Wito kutoka kwa Mfalme
Baada ya chama kumthibitisha, Burnham ataelekea Ikulu ya Buckingham kukutana na Mfalme Charles III, ambaye atamwomba rasmi kuunda serikali mpya na kumwapisha kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao