Chegeni adai kufanyiwa ‘figisufigisu’ Busega

Dk Raphael Chegeni

Muktasari:

Dk Chegeni alisema ana matokeo kutoka kila kituo ambayo hayaendani na yale yaliyowasilishwa CCM, hali aliyosema inaleta wasiwasi wa viongozi kumwandaa ‘mgombea wao’.

Dar/Mikoani. Matokeo ya kura za maoni CCM yameendelea kukumbwa na vituko katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo kutokubali matokeo na kuharibu nyaraka za kura kutokana na malalamiko ya kuwapo mizengwe na upendeleo.

Katika jimbo la Busega, matokeo yaliyotangazwa juzi yalikataliwa na nyaraka kuchanwa.

Mmoja wa wagombea hao, Dk Raphael Chegeni alidai kuongoza kwa kura 12,950 dhidi ya mpinzani wake, Dk Titus Kamani aliyepata kura 10,797.

Dk Chegeni alisema ana matokeo kutoka kila kituo ambayo hayaendani na yale yaliyowasilishwa CCM, hali aliyosema inaleta wasiwasi wa viongozi kumwandaa ‘mgombea wao’.

“Katibu ameshindwa kutangaza matokeo wakati kura halisi zinaonyesha nimeshinda, sasa nini kinachowafanya wasitangaze na hii kuchelewesha ni kumwandalia ushindi mgombea mwenzangu,” alisema chegeni.

Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Hilda Kapaya alisema uchaguzi huo utarudiwa baada ya nyaraka za uchaguzi na matokeo kuchanwa.

“Tumeshindwa kutoa uamuzi kwa maana wagombea walishindwa kuelewana kutokana na kutofautiana kwa matokeo lakini cha kushangaza wajumbe walinyakua karatasi za matokeo, hivyo kushindwa kutambua takwimu sahihi,” alisema Kapaya.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya alisema kuchelewa kwa matokeo hayo kulitokana na baadhi ya vituo kushindwa kuwasilisha matokeo mapema.

Alisema kamati ya siasa ya wilaya ambayo yeye ni mjumbe, ilikaa lakini kikao hicho kilishindwa kumalizika baada ya wajumbe kushindwa kuelewana.

Mufindi Kaskazini: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamoud Mgimwa (12,235), Exaud Kighae (2,343), Raphael  Kalinga (1,520) na Godfrey Ngupula (980).

Mufindi Kusini: Mbunge wa sasa, Mendrad Kigola (7,511), Dickson Lutevele (3,210), Albert Chalamila (1,898) Marcelina Mkini (1,688), Mary Miho (413), Anthony Mpiluka (331) na Wende Ng’ahala (298), Golden Mgonzo (224), Dionis Myinga (214), Alex Sanga (192), Prosper Mfilinge (184), Robert Malangalila (151), Frank Mung’olage (124) na Charles Sanga (121)

Makete: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Binilith Mahenge (8,534), Dk Norman Sigalla (8,211), Bonic Muhami (500), Fabian Mkingwa (466) na Lufunyo Kinda (226).

Njombe Kaskazini: Joram Hongoli (2,233), Gaston Kaduma (1,912), Oscar Msigwa (1,656), Emmanuel Nyagawa (1,083), Avike Kyenga (836), Lemah Hongoli (471), Leila Malekela (365) na Osmond Malekela (103).

Babati Mjini: Mbunge wa sasa, Kisyeri Chambiri (3,722), Ally Msuya (1,758), Haines Darabe (1,758), Ramadhan Slaa (579), Dk Wakat Hindi (551), Ally Sumaye (357), Samo Samo (406), Cosmas Masauda (283) na Sulei Bura (162).

Igalula: Mussa Ntimizi (7,008), Athuman Mfutakamba (4,318) na Hanifa Kitwana (3,935).

Tabora Kaskazini: Almas Maige (9,507), Shaffin Sumar (6,131), Said Kayege (1,319), Clement Mswanyama (1,098), Joseph Kidaha (5,899), Said Juma (737), Humbi Shija (222) na Poul Ngoma (211).

Mwanga: Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (10,459), Joseph Tadayo (9,506), Ramadhan Mahuna (1,019), Karia Magaro (550), Jaffar Mghamba (286), Amaniel Kidali (201) na Baraka Lolila (125).

Longido: Dk Stephen Keruswa (20,085), Joseph Kirunjuu (5,452), Lomayani Logolle (4,579), Phillip Kipasho (4,096), Lee Olduka (1,455), Emmanuel Sirikwa (1,056), Daniel Maralii (970) na Lesion Mollel (277).

Ubungo: Meya wa Jiji, Dk Didas Masaburi (6,068), Kalist Lyimo (2,808), Hawa Ng’humbi  (1,772), Dk Wilson Charles (194), Innocent Mabiki (108), Joseph Massan (378), Jackson Millengo (82), Emmanuel Mboma (93), Zangina S Zangina (134), Timoths Machibya, Jordan Balindo (212) na Cosmas Longino (13).

Kinondoni: Iddi Azzan (6,479), Lusajo Ipambagala (423), John Kalinjuna (116), Macdonald Lunyilija (321), Emmanuel Makene (711), Muhidini Mchoropa (120), Steven Mengele (658), Joseph Mhonda (751), Goodchance Nsangi (164), Mussa Mwanbujule (114), Wangota Salum (1,149) na Michael Wambura (1,212).

Kibamba: Dk Fenela Mukangara (5,576), Issa Mtevu (3,296), John Hugo (319), Pendo Kujerwa (306), Lulu Ng’wanakilala (237), Mechack Sabaya (393), Godvictori Shayo (122), Didas Lunyungu (195) Zakayo Mepuyinywe (73), George Shija (90), Stanslaus Maganga (138) na Felix Mdessa (92.)

Kawe: Kipi Warioba (5,212), Jumaa Pijei (2,497) Coleman Massawe (4,280),  Jery Muro (584), Yusufu Nassoro (559),  Abdallah Majura (392), George Nyaronga (327), Dk Wilson Babyebonela (268), Edmond Lyatuu (293), Elias Nawera (228), John Mayanja (245), Amon Mpanju (112), Amelchiory Kulwizila (175), Tegemeo Sambili (184), Dk Walter Nnko (169), Atulinda Barongo (181), Mtiti Butiku (132), Shiganga George (151), Salum Mohamed (57), Gabriel Munasa (131) na Dickson Muze (94).

Mbulu Vijijini: Fratery Gregory (12,808), Simon Daffi (8,287), Melkiori Nari (921) na Martha Umbulla (327).

Mbeya Mjini: Sambwee Shitambala (4,702) Amani Kajuna (4,544) na Charles Mwakipesile (2,329).

Mbeya Vijijini: Oran Njeza (18,477), Mbunge Lackson Mwanjale (10,240) na Anderson Kabenga (4,073).

Rorya: Mbunge Lameck Airo (20,566) Lukio Ambogo (3,150) na David Wembe (2,870).

Sumbawanga Mjini: Mbunge Aeshi Hilaly (13,611), Anyosisye Kiluswa (1,056), Fortunatus Fwema (727) na Frank Mwalembe (524).

Kondoa Vijijini: Ashatu Kijaji (9,162), Hassani Lubuva (9,113), Moni Lujuo (4,641), Dunga Omari (2,857),  Soloka A. Soloka (2,017), Abasi Kondo (1,239), Issa Omary (1,210), Omary Mdeke (423), Beya Rajabu (409), Kova Ibrahim (324), Abdallah Ally, (309), Haji Kak (229), Abdulli Dello (212) na Ndee Leonad (90).

Kondoa Mjini: Edwin Sanda (2,626), Mbunge Zabein Mhita (1,539) na Ahmedi Nyang’anyi (639), Juma Ikangaa (572), Ally Makoa (555), Ally Happy (243), Juma Fataki (138) na Ally Delo (71).

Chemba: Juma Nkamia (17,406), Paschal Degera (1,777), Khamis Mkotya (1,420), Jumaa Irando (1,064), Yusufu Ndula (1,030), Iddi Kisisa (931), Juliana Shemagembe (892), Frederick Duma (652),  Francis Julius (489), Athumani Hott (266), Paschal Affa (242), Rafael Keresa (197) na Godfrey Sule (81).

Babati Vijijini: Mbunge Vrajilal Jituson (8,523), Daniel Silo (6,222), Dk Vicent Ame (4,660), Damas Nakei (3,249), Faustine Gedi (2,586), Shauri Manda (2,216 ), Omary Kwaang (1,094), Charles Ingi (877) Joseph Kijuu (686), Hassan Kaniki (678), Jamal Mukta (576) na Valerian Sanu (221).

Segerea: Bona Kalua (6,965), Mbunge Dk Makongoro Mahanga (2,381), Scholastica Kizela (6,185), Dasi Kesy (813), Omary Bakari (279), Apruna Umba (125), Mwadeni Liasuka (169), Tuma Salehe (129) Hale Daniel (291), Kazeli Christopher (148), Mboneko Kataruga (221), Pambe Elifuraha (87) na Robart Saanane (73).

Ukonga: Jery Silaa (10,000), Ramesh Patel (7,376) Robert Masegese (548) Maselo Mahende (337), Majura Kaseleko (357), Hussein Mssola (233), Amina Mkono (207), Stenans Magesa (162) Jacob Kasema (174), Hamza Mshindo (150), Amosi Angaya (103), Anton Kalokola (212), Frederick Rwegasila (110), Bachutu Liyasuta (97), Labson Jordan (99) na Moses Elias (79).

Imeandikwa na Joseph Lyimo, Geofrey Nyang’oro, Christopher Lilai, Shaban Lupimo, Moses Mashalla, Sylvia Kombe, Beatrice Moses, Faustine Fabian, Emma Kalalu, Joseph Lymo, Shakila Nyerere, Waitara Meng’anyi na Mussa Mwangoka.